Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:59

Afisa wa juu wa uchaguzi Georgia amkosoa Rais Trump


Waziri wa Mambo ya Nje wa jImbo la Georgia Brad Raffensperger
Waziri wa Mambo ya Nje wa jImbo la Georgia Brad Raffensperger

Rais wa Marekani anachosema ni “makosa ya wazi” kuhusu dosari za uchaguzi huko Georgia, afisa wa juu wa uchaguzi  wa jimbo hilo amesema Jumatatu baada ya kukataa maombi ya Trump wikiendi kumtafutia kura zaidi kujazia kura alizokosa katika uchaguzi katika jimbo hilo ambazo zilipigiwa kumchagua Rais Mteule Joe Biden.

Waziri wa Mambo ya Nje wa jimbo hilo Brad Raffensperger, ambaye ni afisa wa uchaguzi wa jimbo hilo la kusini amekiambia kituo cha televisheni cha ABC kuwa wakati wa mazungumzo ya simu yaliodumu kwa saa moja na Trump, ilikuwa dhahiri kwamba rais anaendelea na nadharia yake isiyokuwa na msingi kuhusu wizi wa kura, alidai kwamba kura za wajumbe 16 za jimbo alimpa kimakosa Biden.

Rais mteule Joe Biden
Rais mteule Joe Biden

“Yeye ndiye alikuwa anaongea zaidi. Sisi tulikuwa tunamsikiliza,” alisema Raffensperger. “Takwimu alizokuwa nazo si sahihi… ana takwimu mbaya.”

“Kwa miezi miwili iliyopita, tumekuwa tukipambana na uvumi huu,” Raffensperger amesema. “Na ilikuwa wazi mapema kabisa tulikuwa tumejibu kila nadharia iliyotolewa. Lakini Rais Trump anaendelea kuziamini… Sisi tunaamini ukweli ndio muhimu.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Georgia Brad Raffensperger akihudhuria mkutano wa maafisa wa uchaguzi mjini Savannah, Georgia, Disemba. 11, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Georgia Brad Raffensperger akihudhuria mkutano wa maafisa wa uchaguzi mjini Savannah, Georgia, Disemba. 11, 2019.

Trump ambaye amekataa kukubali kushindwa na Biden, ameendelea mashambulizi Jumatatu juu ya matokeo ya uchaguzi kwa njia ya Twitter, akisema jioni, atatoa “takwimu sahihi,” atakapo kwenda Georgia kufanya kampeni kwa ajili ya wagombea wa wawili Warepublikan kwa viti vya seneti wanaokabiliana katika kinyang’anyiro hicho na wagombea wa chama cha Demokratik Jumanne.

“Vipi utathibitisha uchaguzi wakati nambari zinazo thibitishwa zilihakikiwa kimakosa,”Trump alisema hayo katika maoni yake ya Twitter ambayo yamewekewa alama “yanapingwa.”

"Hivyo kile ninachotaka ni hiki, kupata kura 11,780, ikiwa ni moja zaidi kuliko tulichopata" Trump alimwambia afisa wa uchaguzi wa ngazi ya juu, Waziri wa Mambo ya Nje wa jimbo hilo Brad Raffensperger katika mazungumzo yaliyo rikodiwa na kuchapishwa na gazeti la Washington Post Jumapili mchana.

Katika mazungumzo ya saa moja, Trump alikuwa kati ya kumkosoa Raffensperger na kumpaka mafuta na Mwanasheria Mkuu wa ofisi yake Ryan Germany. Rais alipinga usahihi wa hesabu tatu tofauti za kura huko Georgia zilizokuwa zinaonyesha Biden ni Mdemokratik wa kwanza mgombea urais kulichukua jimbo hilo tangu 1992.

Siku ya Jumapili, Trump alisema kupitia akaunti yake ya Twitter, “Niliongea na Waziri wa Mambo ya Nje Brad Raffensperger Jumapili kuhusu Kaunti ya Fulton na udanganyifu wa kura Georgia. Lakini hakuwa tayari au hakuweza kujibu maswali kama vile “kura zilizo fichwa chini ya meza,” wizi, uharibifu wa kura, wapiga kura kutoka majimbo mengine, wapiga kura marehemu, na mengineyo. Hana taarifa yoyote!”

Raffensperger alijibu saa chache baadae, “Kwa heshima, Rais Trump : KIle unachosema siyo kweli. Ukweli utajitokeza.”

Marekani inayotumia mfumo wa demokrasia sio ya moja kwa moja, Biden, kwa kushinda kura za wananchi, alishinda kura zote 16 za kura za wajumbe kufikia kura 306 alizomshinda Trump ambaye alipata kura 232 katika Electoral College.

Siku ya Jumatano, mkutano wa pamoja wa mabaraza mawili ya bunge ambapo Makamu wa Rais Mike Pence ataongoza. Angalau dazeni ya Maseneta wa Republikan wamesema wataungana na idadi isiyojulikana ya Wawakilishi kupinga kuthibitisha kura za Wajumbe zilizopigwa kumchagua Biden.

XS
SM
MD
LG