Mgombea urais wa chama cha Democratic Joe Biden amechukua uongozi wa kura chache dhidi ya Rais Donald Trump katika majimbo muhimu yenye ushindani mkali ya Georgia na Pennyslvania, hivyo anaelezewa kuwa anaelekea kupata kura za kutosha za wajumbe kutangazwa mshindi.
Makamu rais wa zamani Biden ambaye hivi sasa anaongoza katika kura za wananchi pia ana kura 253 za wajumbe dhidi ya 214 za Trump. Mgombea anahitaji kupata kura za wajumbe 270 ili kushinda urais na kuongoza kwa kipindi cha miaka minne.
Zoezi la kuhesabu kura bado linaendelea katika majimbo ya Arizona na Nevada, ambako Biden anaongoza. Mfumo wa kura za wajumbe Marekani unayaruhusu mshindi wa kura wa wananchi katika kila jimbo anapata kura za wajumbe wote wote isipokuwa kwa majimbo mawili tu ya Maine na Nebraska ambapo wajumbe wanaamuliwa kulingana na kanuni za majimbo hayo.