Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:08

Biden aahidi kuliunganisha taifa


Rais mteule Joe Biden
Rais mteule Joe Biden

Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, ambaye ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais, ameahidi atakuwa “rais ambaye hataigawanya, bali ataiunganisha” nchi hii katika hotuba yake kwa taifa Jumamosi usiku kutoka Wilmington, Delaware.

Akirejea hotuba zake za zamani, Biden amesema ni “wakati wa kuepuka siasa za chuki, kupunguza jazba, kukutana tena, na kusikilizana kati yetu.”

Biden amewasihi wafuasi wake wawasiliane na wale ambao hawakumpigia kura, na amekiri kuna wenye masikitiko wale waliomuunga mkono Rais Donald Trump.

“Nimeshindwa mara kadhaa,” Biden amesema, “sasa, kila mmoja ampe mwenzake fursa.”

Rais huyo mteule pia amesema kuwa Jumatatu atazindua kikosi kazi cha COVID-19 “kilichojikita katika sayansi” kuanza kazi ya kudhibiti janga hilo, ambalo takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonyesha limeambukiza zaidi ya Wamarekani milioni 9.8 na kuua zaidi ya watu 237,000.

Akiwa anajulikana katika siasa za Washington kwa karibu nusu karne, Biden anatarajiwa kuapishwa Januari 20, pamoja na Makamu wa Rais Mteule Kamala Harris, hivi sasa ni Seneta wa California.

Biden alitambulishwa Jumamosi usiku na Harris, binti wa wahamiaji ambaye atakuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani Mweusi na mwenye asili ya India kuhudumu nafasi ya makamu wa rais.

“Wakati demokrasia yetu ilipokuwa kwenye kura katika uchaguzi huu, na roho ya Marekani kuwa hatarini na dunia ikiangalia, imeleta siku mpya kwa Marekani,” amesema Harris kuwaambia umati wa watu waliokuwa wako nje wakiwa mbalimbali.

Aliwashukuru wapiga kura nchini kote kwa kujitokeza kwa idadi kubwa na kufikisha “ujumbe uliowazi : mmechagua matumaini, umoja, heshima, sayansi na ndio, ukweli,” alisema. “Mmemchagua Joe Biden kuwa rais ajaye wa Marekani.”

Harris alivalia mavazi meupe kuenzi haki ya wanawake kupiga kura na kufungua hotuba yake kwa kutoa heshima kwa Mwakilishi wa Georgia hayati John Lewis, shujaa wa haki za kiraia.

Kadhalika alitoa heshima kwa mama yake, Shyamala Gopalan Harris, na vizazi vya wanawake waliokuwepo kabla yake.

“Wakati nikiwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hii, sitakuwa wa mwisho,” alisema. “Kila msichana anayeangalia usiku wa leo anaona hii ni nchi ambayo chochote kinawezekana.”

XS
SM
MD
LG