Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:38

Zoezi la kupiga kura lafikia kileleni Marekani


Wapiga kura wakiwa katika shule ya Stone inayotumika kama kituo cha kupiga kura mjini Hillsboro, Jimbo la Virginia Novemba 3, 2020. (Photo by ANDREW CABALLERO-REYNOLDS / AFP)
Wapiga kura wakiwa katika shule ya Stone inayotumika kama kituo cha kupiga kura mjini Hillsboro, Jimbo la Virginia Novemba 3, 2020. (Photo by ANDREW CABALLERO-REYNOLDS / AFP)

Mamilioni ya Wamarekani wanatarajiwa kushiriki Jumanne katika Uchaguzi Mkuu unaosemekana ni wa kihistoria kutokana na ushindani mkubwa uliyopo na idadi kubwa ya watu waliokwisha jitokeza kupiga kura mapema.

Leo Wamarekani wanapiga kura kumchagua rais, wajumbe wa mabaraza ya bunge la taifa pamoja na wale wa mabunge ya majimbo na serikali za mitaa.

Wachambuzi na vyombo vya habari wanaripoti kwamba Wamarekani wanahasira na wamegawika kuliko wakati wowote ule tangu vita vya Vietnam miaka 1970.

Kutokana na hali hiyo na hasa janga la virusi vya Corona majimbo yameruhusu watu kupiga kura mapema kwa kulegeza masharti ya kupiga kura kwa njia ya posta na upigaji kura wa mapema.

Matokeo yake kuna Wamarekani milioni 100 waliokwisha piga kura zao Ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kushuhudiwa.

Rais Donald Trump (kulia) na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden
Rais Donald Trump (kulia) na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden

Kinya’ganyanyiro cha kugombania kiti cha rais kinatazamiwa kuwa ushindani katika majimbo 10 yanayo fahamika kama majimbo yenye ushindani mkubwa. Wakazi wa majimbo hayo huwa wanabadilisha uungaji mkono wao kila msimu wa uchaguzi.

Safari hii utafiti wa maoni unaonyesha Joe Biden Mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik anaongoza katika majimbo hayo ya ushindani hasa ya Pennsylvania, Wisconssin, Michigan Florida na Iowa, majimbo ambayo Trump alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2016.

Uchaguzi wa rais wa Marekani unafuata mfumo wa kipekee ambapo kura za wananchi hazimchagui rais moja kwa moja bali uamuzi wa mwisho wa kumchagua huchukuliwa na Kura za Wajumbe maarufu kama Electoral College.

Kuna wajumbe 538 kwenye baraza hilo wanaowakilisha majimbo yote 50 ya taifa hili na ili kuweza kushinda mgombea anahitaji kupata kura 270 za wajumbe wa uchaguzi.

Mbali na kumchagua Rais wapiga kura wanawachagua wajumbe wa bunge la 117. Kuna viti 35 vya Baraza la Seneti vinavyogombaniwa pamoja na viti vyote 435 vya Baraza la Wawakilishi.

Wademokrats kwa hivi sasa wanaudhibiti wa Baraza la Wawakilishi na wachambuzi wanasema hakuna dalili watapoteza udhibiti huo.

Mashindano wanasema wachambuzi yako katika Baraza la Seneti ambako Wadeokrats wanahitaji kati ya viti vitatu au vinne kuweza kuchukua udhibiti wa baraza hilo linaloshikiliwa hivi sasa na Warepublican.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 kulingana na takwimu kuna Wamarekani milioni 230 waliokwisha andikishwa kupiga kura na kutokana na idadi ya waliopiga kura mapema wachambuzi wanasema huenda mwaka huu idadi ya jumla ya wapiga kura itakuwa juu kabisa kuwahi kushuhudiwa. Katika uchaguzi wa mwisho wa 2016 watu milioni 138 walipiga kura.

Mbali na kuvunjwa kwa rikodi hizo kulingana na kituo cha kufuatilia matumizi ya kampeni Center for responsive politics kampeni za vyama vyote viwili Wademokratik na Warepublikan zimevunja rikodi upande wa matumizi ambapo kila mgombea ametumia zaidi ya dola bilioni 6.6, Ikiwa dola bilioni 2 zilizotumiwa na Trump na Clinton.

Kwa ujumla kampeni za uchaguzi mwaka huu kufuatana na utafiti huo zimetumia dola bilioni 14 ambapo dola bilioni 7 zilitumiwa kugombania viti vya bunge la taifa.

XS
SM
MD
LG