Masuala yanayo jitokeza hivi sasa ni idadi gani ya wapiga kura watakao jitokeza kesho Jumanne, na ikiwa matokeo yatatangazwa hapo kesho au itabidi kusubiri mamilioni ya kura zilizotumwa kwa njia ya posta kuweza kujua nani atakuwa rais ajae wa Marekani.
Wagombea kiti cha rais wote Rais Donald Trump na mpinzani wake Makamu Rais wa zamani Joe biden wanafanya mikutano yao ya mwisho Jumatatu kuwavutia wapiga kura ambao watashiriki kwenye uchaguzi huo wa kihistoria.
Kitu kisicho fahamika ni idadi gani ya wapiga kura kati ya milioni 230 wanaoweza kupiga kura watajitokeza. Hadi hii leo zaidi ya wapiga kura milioni 95 wameshapiga kura zao kwa njia ya posta au kura ya mapema Ikiwa ni idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa, na ni zaidi ya asilimia 67 ya watu wote walioshiriki kwenye uchaguzi wa 2016. Na safari hii kwa sehemu kubwa inatokana na wasiwasi wa ugonjwa wa COVID-19, na ushindani mkubwa uliyopo na wasiwasi wa wizi wa utumiaji wa njia ya posta ulioelezwa na Rais Trump.
Kila mmoja kati ya kampeni za wagombea wote wawili anadai ushindi ni wao. Jason Miller mshauri muandamizi wa kamoeni ya Trump anadai mgombea wake amewpanua uungaji mkono wa wafuasi wake wakuu hasa miongoni mwa waareani wusi na wenya asili ya nchi za amerika ya kusini katika majimbo ambyo kihistoria ni ngome ya wademokrat.
Jason Miller mshauri muandamizi wa kampeni ya Trump anaeleza : "Umbo la wapigaji kura limebadilika kabisa. Namna watu wanavyounga mkono kampeni imebadilika pia safari hii. Kutokana na kwamba Joe Biden amelazimika kurudi Minnesota, jimbo ambalo WarepubliKan hawajapata kushinda tangu 1972, inaonyesha jinsi walivyo na wasiwasi muelekeo wa majimbo unavyobadilika."
Wademokratik kwa upande wao wanasema njia yao kuelekea ushindi inabadilika pia, kwani majimbo ambayo kawaida ni ngome ya Warepublikan yamekuwa majimbo yenye ushindani mkubwa hadi siku ya uchaguzi.
Biden na mgombea wake mwenza Kamala Harris wametembelea Texas, Georgia na Iowa majimbo amabyo yalimuunga mkono Trump kwenye uchaguzi wa 2016.
Anita Dunn mshauri muandamizi wa kampeni ya Biden anasema idadi ya watu watakao jitokeza itavunja rikodi zote kwa sababu watu wamehamaishiwa kutaka kuona mageuzi.
Anita Dunn Mshauri muandamizi wa kampeni ya Biden anatema : "Ukitizama jinsi watu walivyo hamasika kwa kiwango amacho tumeshuhudia mnamo upigaji kura wa awali ni ishara kwamba watu wengi watakwenda kupiga kura. Na tutafahamu siku ya uchaguzi kwamba idadi kubwa ya watu kuwahi kutokea huenda wakajitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi huu kwa sababu wanataka mabadiliko."
Wachambuzi wanasema upande utakao wavutia wapiga kura wengi kujitokeza ndio huenda ukawa mshindi .
Hata hivyo haifahamiki wakati gani matokeo kamili yatajulikana baada ya uchaguzi kwa hivyo Wamarekani watalazimika kusubiri kwa muda kuweza kujua matokeo ya uchaguzi huu utakaokumbukwa kwa miaka mingi ijayo.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC