Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:19

Wamarekani waridhika na mdahalo wa mwisho kati ya Trump na Biden


Watu wakiangalia mdahalo kati ya Rais Donald Trump katika magari yao.
Watu wakiangalia mdahalo kati ya Rais Donald Trump katika magari yao.

Wamarekani wameridhika na namna mdahalo wa pili na wa mwisho kati ya Rais Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden ulivyofanyika Alhamisi usiku.

Hata hivyo wachambuzi wanasema hawadhani mdahalo huo yameweza kubadili maoni ya wapiga kura.

Wagombea hao wawili waliweza kueleza misimamo yao bila ya kuingiliana kati kinyume na jinsi ilivyofanyika kwenye mdahalo wa kwanza na wamezungumzia kuanzia masuala ya janga la COVID-19, huduma za afya hadi usalama wa taifa.

Nashville Tennessee

Mdahalo huo uliofanyika mjini Nashville Tennessee, chini ya wiki mbili kabla ya Wamarekani hawajapiga kura, ingawa idadi ya waliopiga kura ya awali imefikia zaidi ya milioni 40 hapo jana, Ikiwa ni idadi kubwa ya upigaji kura wa mapema kuwahi kufanyika hapa nchini.

Swali la Kwanza

Swali la kwanza lilikuwa COVID-19 na Trump alijitetea juu ya namna alivyo kabiliana na janga hilo.

Trump alisema : Ni janga lililotokea kote duniani. Ugonjwa umesambaa kila mahali. Tunaona kuongozeka tena ugonjwa huko Ulaya na maeneo mengine mengi."

Akizungumzia nini atakacho fanya anasema huenda kuna chanjo ikawa tayari karibuni. Lakini Biden amesema hiyo itakuwa imechelewa kwa Wamarekani 220,000 walio kwisha fariki.

Biden

Biden alieleza : "Yeyote anaehusika na idadi hiyo kubwa ya vifo hafai kubaki kuwa rais wa Marekani.

Wagombea hao wawili walilaumiana kuhusu ulaji rushwa Trump akijaribu kumtuhumu Biden kwa namna alivyonufaika na mipango ya biashara ya kijana wake, Hunter huko Ukraine na Rashia.

Trump

Trump aeleza : "Barua pepe zote, barua pepe zilizokuwa na habari mbaya kuhusu kiwango kikubwa cha fedha uliokuwa unapata wewe na familia yako. Na Joe wewe ulikuwa makamu wa rais wakati haya yote yalikuwa yanafanyika." Naye Biden alikanusha vikali tuhuma hizo.

Biden alisema : "Sijapata kuchukuwa hata senti moja kutoka chanzo cha kigeni maishani mwangu. Tumearifiwa kwamba huyu rais alilipa mara 50 zaidi ya kodi nchini china ambako ana akaunti za siri za benki na China, akifanya biashara nchini China."

Trump alijitetea akisema akaunti hiyo haikuwa jambo la siri na amefanya biashara kote duniani. Alikanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba hakulipa au alilipa kodi kidogo sana Marekani mnamo miaka ya karibuni akisema amelipa kodi ya awali ya mamilioni ya dola.

Kwa ujumla wachambuzi wanasema mjadala ulifanyika vizuri na Jeremy Mayer wa chuo kikuu cha George Mason anasema wagombea wote walifanya vizuri na Biden alimaliza kwa nguvu mwisho wa dakika 90 za mdahalo.

Chuo Kikuu cha George Mason

Mayer wa chuo kikuu cha George Mason amesema : "Suala la mwisho walilomuliza, ni ujumbe gani utatoa kwa wananchi ambao hawakukupigia kura pindi ukishinda.? Ulikuwa ni ujumbe wa kuwaunganisha watu kinyume na mivutano na ugomvi tunaoshuhudia katika siasa za nchi yetu.

Anasema hata hivyo Trump hakukubali kushindwa kwani alijuwa la kufanya nalo ni kujaribu kumchafua Biden na kashfa kuhusiana na kijana wake.

Kilichobaki hivi sasa ni kupambana katika majimbo karibu 6 yenye ushindani ambayo huwenda yakamua nani ataapishwa rais wa Marekani hapo Januari 20 mwakani.

XS
SM
MD
LG