Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:57

Wabunge wa Marekani wapinga wazo la kutokuwepo kukabidhiana madaraka kwa amani


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Viongozi wa vyama vyote viwili katika Bunge la Marekani wamepinga wazo la uwezekano wa rais Donald Trump kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa Novemba 3.

Rais Trump kwa mara nyingine Alhamisi alihoji iwapo upigaji kura kwa njia ya posta utafanyika kwa njia ya haki na huru. Ukusanyaji wa maoni wa hivi karibuni unaonyesha kwamba idadi kubwa zaidi ya Wademokrati watapiga kura kwa njia ya posta kuliko Warepublican.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Matamshi ya Trump yametolewa wakati vyama vyote viwili vinajitayarisha kwa uwezekano wa kuwepo na ushindani mkali wa uchaguzi wa rais.

Tofauti hiyo kubwa iliyopo ya upigaji kura kwa njia ya posta imewasababisha wachambuzi wa masuala ya kisiasa kueleza kwamba huenda ikapelekea mfarakano katika matokeo ya uchaguzi.

Katika hali hiyo huenda Rais Trump akadai ushindi baada ya matokeo ya awali kutangazwa, lakini hatimaye akashindwa na mpinzani wake wa chama cha Demokratik Joe Biden kutokana na kura zilizopigwa kwa njia ya posta siku chache baadae.

Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden
Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden

Kutokana na taswira hiyo mkuu wa baraza la Senate Mrepublican Mitch McConnell alitoa tarifa alhamisi usiku kuwahakikishia wamarekani kwamba mshindi wa uchaguzi wa Novemba 3 atachukua madaraka kama ilivyopangwa hapo mwezi Januari.

Zogo hili lote limetokana na Trump kwa mara nyingine kusema kwamba kutakuwepo na ubadhirifu na njama katika upigaji kura kwa njia ya posta, akitabiri kwamba huwenda kukawa na mashtaka ya kisheria juu ya matokeo na hatimaye Mahakama ya Juu ikalazimika kuamua nani ni mshindi.

Hiyo ndio sababu moja kuu Trump anataka kumteua kwa haraka mtu atakaye chukua nafasi ya Jaji wa mrengo wa kushoto Ruth Bader Ginsburg aliyefariki wiki iliyo[pita.

Donald Trump anaeleza : "Ninadhani jambo hili litafikishwa mbele ya mahakama kuu. Na ninadhani ni muhimu kabisa kuwepo kwa majaji wote 9."

Wachambuzi wanasema kwamba ingawa hakuna ushahidi wa ubadhirifu mkubwa wa upigaji kura kwa njia ya posta kama rais anavyodai, lakini mara nyingi kuna uwezekano kura hizo zikatupiliwa mbali kutokana na kasora katika kukamilisha vyema vyeti hivyo.

Akitoa ushahidi mbele ya kamati ya bunge mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai FBI Christopher Wray anasema wanachukulia kwa dhati kughushi kwa namna yeyote katika upigaji kura.

Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray
Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray

Wray anaeleza kuwa : "Hatujapata kushuhudia aina yeyote ya kughushi katika upigaji kura uliopangwa kitaifa katika historia ya nchi yetu kati wa uchaguzi mkuu, ikiwa ni kwa njia ya posta au vinginevyo.

Sam Berger mchambuzi wa masuala ya kisiasa katika kituo cha American Progress anasema jukumu la mahakama ya juu katika hali hiyo yote haijulikani bado.

Berger anaeleza zaidi : Natumai hatutakuwa katika hali ambayo tutaiomba mahakama kuamua juu ya kesi itakayo amua matokeo ya uchaguzi. Ninadhani hilo litakuwa tatizo kwa demokrasia.

Mara ya mwisho mahakama ya juu ilibidi kuingilia kati ni wakati wa uchaguzi wa rais wa mwaka 2000 kutokana na ugomvi wa kuhesabu upya kura katika jimbo la Florida na kumpatia ushindi Mrepublican George W Bush, dhidi ya Makamu Rais wa zamani Albert Al-Gore kwa kura moja tu. Gore alikiri kushindwa ingawa alipata wingi wa kura.

Rais mstaafu George W. Bush na Makamu wa Rais wa zamani Albert Al-Gore

Trump alipoulizwa iwapo atakubali kukabidhi madaraka kwa amani akishindwa uchaguzi alisema ”tutaona kitakachotokea”

Kutokana na mvutano mkubwa uliyopo hivi sasa hapa nchini pande zote mbili za kisiasa zinahofia kuwepo mabishano makali juu ya matokeo ambayo huenda yakasababisha mapambano ya kisiasa kati ya wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia na kushoto.

XS
SM
MD
LG