Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alisema mwezi uliopita kuwa ameanzisha mchakato wa siku 30 katika baraza hilo utakopelekea kurejesha vikwazo vya UN dhidi ya Iran Jumamosi jioni ambavyo pia vitaendeleza marufuku ya silaha za kawaida dhidi ya Tehran kutomalizika Octoba 18.
Lakini wanachama 13 kati ya 15 wa Baraza la Usalama wanasema hatua ya Washington ni batili kwa sababu Pompeo ametumia utaratibu uliokubaliwa mwaka 2015 wa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu, ambapo Marekani uiijitoa mwaka 2018, shirika la habari la Uingereza Reuters limeripoti.
“Litakalo jitokeza ni kukosekana uthibiti iwapo au siyo mchakato huo … ulikuwa kwa kweli umeanzishwa na unafungamana kama ulivyoandikwa iwapo au siyo (vikwazo) hivyo kusitishwa…vinaendelea kutekelezwa,” Guterres ameandika katika barua aliyoituma kwa baraza hilo, ambayo shirika la habari la Reuters wameiona.
“Haipaswi kwa Katibu Mkuu kuendelea kama kwamba hali hiyo ya kukosekana uhakika haipo,” amesema.
Maafisa wa UN hutoa msaada wa kiuongozi na ufundi kwa Baraza la Usalama katika kutekeleza vikwazo hivyo na Guterres huwateua wataalam wa kujitegemea kufuatilia utekelezaji huo.
Katibu Mkuu amesema “hadi kupatikana ufafanuzi” juu ya hali ya vikwazo hivyo dhidi ya Iran, hatochukuwa hatua yoyote kutoa msaada huo.