Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:34

Kiongozi wa kiroho wa Iran amshambulia Rais Donald Trump


Rais Donald Trump na Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei
Rais Donald Trump na Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei

Kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, amesema Rais wa Marekani, Donald Trump, ni mpubavu ambaye anajidai kuwaunga mkono Wairan, lakini, mwishowe, atawachoma kisu chenye sumu.

Matamshi hayo ya Khamenei ni mwendelezo wa kauli zake zilizo na msimamo mkali, na aliyatoa wakati wa hutba ya sala ya Ijumaa ikiwa ni mara ya kwanza mjjini Tehran, tangu mwaka 2012.

Khamenei amesisitiza kwamba umati mkubwa wa watu, ulijitokeza, ili kuhudhuria mazishi ya jenerali wa jeshi aliyeuawa katika shambulizi lililotekelezwa na Marekani mapema mwezi Januari 2020.

Amesema pamoja na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili nchi hiyo, inaonyesha jinsi raia wa Iran wanavyounga mkono utawala wake.

Amesema kwamba kifo cha Jenerali Qassem Soleimani, ni pigo kubwa kwa vita dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State, kwa sababu, kama kamanda, alionyesha uongozi bora katika kupambana na wanamgambo hao.

Katika siku za karibuni, kumeshuhudiwa maandamano makubwa kwenye barabara za Tehran, kufuatia kutunguliwa kwa Ndege ya shirika la Ndege la Ukraine, ambayo, viongozi wa Iran, wamekiri kwamba ilitunguliwa kwa makosa.

Watu wote 176 waliokuwa wakisafiri ndani ya ndege hiyo waliuawa. Sala ya Ijumaa ilihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Iran, mara kwa mara walikatiza hotuba yake wakisema, Mungu ni Mkubwa.

XS
SM
MD
LG