Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:16

Hatua ya Marekani kumuua Jenerali wa Iran yaibua wito wa kulipiza kisasi na wengine kujizuilia


Marehemu Meja Jenerali Qassem Soleimani
Marehemu Meja Jenerali Qassem Soleimani

Kufuatia shambulizi la anga lililofanywa na Marekani kumuua kiongozi wa Jeshi maalum la Quds la Iran nchini Iraq wito umetolewa na pande mbili moja ikitaka nchi hiyo kujizuia na wengine wakitaka ilipize kisasi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ameyaita mauaji hayo ya Jenerali Qassem Soleimani “ni kitendo cha kigaidi na kinaingilia uhuru wa nchi ya Iraq.”

Wizara ya Ulinzi

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetetea hatua hiyo ya kumuua Soleimani kwa sababu “alikuwa anajihusisha na mipango ya kuandaa mashambulizi dhidi ya wanadiplomasia na wafanyakazi wa Marekani walioko Iraq na maeneo yote.” Jenerali huo alikuwa ni mwanamikakati muhimu wa kivita kwa taifa la Iran.

“Kufa shahidi kwa Soleiman kutaifanya Iran kuwa na maamuzi muhiimu katika kupinga kuenea kwa uvamizi wa Marekani na kutetea maadili yetu ya Kiislam,” Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema katika tamko lake. “Bila ya mashaka yoyote, Iran na nchi nyingine zinazotafuta uhuru wake katika eneo la Mashariki ya Kati watalipiza kisasi.

Spika wa Baraza la Wawakilishi

Wakati huohuo Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema shambulizi hilo limefanywa “bila ya kutaka ushauri kutoka Bunge la Marekani na ni kitendo cha hatari “kinachoweza kuchochea kuongezeka kwa hali ya hatari yenye uvunjifu wa amani.” Amesema “Marekani – na dunia – haitaweza kuhimili kuwepo ongezeko la migogoro hadi kufikia hali isiyoweza kupatiwa suluhu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Dominic Raab amezitaka pande zote katika mgogoro huo kupunguza mvutano.

Kikundi cha Hamas

Msemaji wa kikundi cha Hamas cha Palestina amesema kuuawa kwa jenerali “kunafungua milango ya kila kinachowezekana kufanyika katika eneo hilo, na siyo tena kuwepo utulivu na amani.” Bassem Naim amesema “Marekani ndiyo inayohusika na hilo.”

China

Msemaji wa serikali ya China alisema kuwa China “inapinga utumiaji wa majeshi katika mahusiano ya kimataifa.” Ameongeza, “tunazitaka pande zote husika, na hasa Marekani, kujizuia na kupunguza kuongezeka kwa mgogoro huo.”

Baraza la Seneti

Seneta wa Marekani Jim Risch, Mwenyekiti wa Warepublikan katika kamati ya Seneti ya Mambo ya Nje amesema kupitia ujumbe wa Twitter kuwa “leo haki imefanyika,” akiongeza, “Kama nilivyokuwa nimeionya serikali ya Marekani huko nyuma, wasifanye makosa kuchukulia kujizuia kwetu kuchukua hatua katika mashambulizi walioyafanya siku za nyuma kuwa ni udhaifu wetu.”

“Huu ni uchochezi mkubwa wa mgogoro huu katika eneo ambalo tayari ni hatarishi,” amesema Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, mgombea kwa urais wa Chama cha Demokrat.

Rais Trump

Rais wa Marekani Donald Trump, anasema Biden, “amerusha baruti katika moto, na anajukumu la kutoa maelezo kwa watu wa Marekani juu ya mkakati na mpango wa kuhakikisha vikosi vyetu na wafanyakazi wa ubalozi, watu wetu na maslahi yetu, yote hapa nchini na nchi za nje, na washirika wetu katika eneo lote la Mashariki ya Kati na maeneo mengine.

Moshen Rezaei, kamanda wa zamani wa kikosi cha jeshi la Mapinduzi la Iran, amesema “italipiza kisasi kwa nguvu zote dhidi ya Marekani.”

XS
SM
MD
LG