Shirika la habari la ILNA, limenuku chanzo cha Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknologia, kikisema hatua hiyo iliamrishwa na viongozi wa usalama nchini humo.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa hatua hiyo ya kufunga huduma ya intaneti inahusu mikoa ya Alborz, Kuderstan, na Zanjan katikati na magharibi ya Iran na maeneo ya mbali ya kusini mwa nchi hiyo.
Kulingana na taarifa za mitandao ya kijamii na baadhi ya ndugu wa watu waliouawa katika maandamano ya mwezi Novemba 2019 ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta, wameitisha maandamano mengine Alhamisi, kuwakumbuka wale waliopoteza maisha katika vuguvugu hilo.
Vyanzo mbalimbali vya habari vinaeleza waandamanaji hao waliuawa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano.
Shirika la haki za binadamu Amnesty International limesema watu 304 waliuawa wakati wa maandamano ya mwezi Novemba.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.