Maandamano hayo yanayoendelea katika miji mbali mbali yameitikisa Iran kwa wiki nzima.
Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa wapenda mageuzi wamehoji iwapo baadhi ya maadui zao waconservative nchini humo walikuwa wamehusika katika kuchochea maandamano hayo – wakishuku kuwa walikuwa wamefanya hivyo kuidhoofisha serikali ya Rais Hassan Rouhani.
Vyombo vya habari ambavyo vinafadhiliwa na kikosi maalum cha jeshi cha Republican Guards (IRGC) nchini Iran wiki hii vilitangaza mahojiano na waandamanaji wenye hasira waliokerwa na kupanda kwa bei za bidhaa.
Pia waandamanaji hao walikuwa wakikosoa usimamizi wa Rouhani katika kuendesha uchumi, wakimlaumu kutokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu na kushindwa kuleta maboresho ya kiuchumi ambayo alikuwa ameahidi.
Baadhi ya mitandao ya kijamii ikiwemo Avant TV, zilikuwa zimeanzishwa hivi karibuni—ikilinganishwa na vituo vya habari venye kuisaidia serikali vilivyoibuka bila ya kutegemewa wakati na baada ya shinikizo la wanaotaka demokrasia mwaka 2009.