Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:35

Wanawake Afrika Mashariki waendelea kuleta mabadiliko


Roselyn Akombe (kati) akiwa amesimama wakati Rais Uhuru Kenyatta (watatu kulia) akipokea shahada ya ushindi wa matokeo ya uchaguzi, ambao ulibatilishwa baadae na Mahakama ya Juu nchini Kenya
Roselyn Akombe (kati) akiwa amesimama wakati Rais Uhuru Kenyatta (watatu kulia) akipokea shahada ya ushindi wa matokeo ya uchaguzi, ambao ulibatilishwa baadae na Mahakama ya Juu nchini Kenya

Mwaka 2017 kama ilivyo katika miaka mingine, wanawake wameendelea kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali.

Wako wanawake waliokuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2017.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:01 0:00

Nchini Rwanda na Kenya, mwaka 2017 ulikuwa mwaka wa uchaguzi. Wanawake hawakuwa nyuma kujitokeza kugombania nafasi za kisiasa, ama kushiriki katika usimamizi wa uchaguzi.

Mwanamke wa kwanza tunaye mtupia jicho ni Mnyarwanda Diane Shima Rwigara mwenyeumri wa miaka 35 tu, alijitokeza kuwania urais na kuwa mpinzani wa Rais Paul Kagame, wachambuzi wengi wakisema si jambo la kawaida.

Diane ambaye pia ni mfanyabiashara na mwanaharakati wa haki za binadamu, akiwa ni mgombea pekee wa kike aliondolewa katika mbio hizo na tume ya uchaguzi ya Rwanda, kwa madai ya kutokamilisha idadi ya wadhamini 600 waliohitajika na baadhi ya wale aliowaorodhesha 572 tayari walishafariki.

Uamuzi huo wa tume ya uchaguzi ulikosolewa sana kimataifa. Baadaye alikamatwa pamoja na wanafamilia yake kwa mashitakaya kugushi na kukwepa kodi.

Mwanamke mwengine aliyefanya jambo la kukumbukwa ni Roselyn Akombe, ambaye alijiuzulu wadhifa wake waukamishna wa tume huru ya uchaguzi yna mipaka ya IEBC baada ya kutokea mivutano ya kisheria na kashfa kuwa tume hiyo haikusimamia ipasavyo uchaguzi wa Kenya, ule wa Agosti 8, 2016 na wa marudio uliofanyika Oktoba 26.

Akiwa jijini New York mara baada ya kukimbia Kenya, Akombe alitoa taarifa akielezea kwamba uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 hauwezi kufikia vigezo vinavyohitajika. Pia akaweka wazi kwamba kukimbia kwake Kenya, ni kwa sababu ya kuhofia maisha yake. Kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa wakati huo, Akombe anaingia katika orodha ya wanawake wa kukumbukwa kwa mwaka 2017.

Mwanamke mwingine wa kukumbukwa kwa mwaka 2017 ni Rebecca Gyumi, ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za mtoto wa kike. Kupitia taasisi yake ya Msichana Initiative, alifanikiwa kuishinda serikali katika kesi ya kupinga kipengele cha sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa chini ya miaka 18 kwa ridhaa ya wazazi.

Kutokana na hilo Rebecca alipata tuzo mbalimbali kutoka mashirika ya kimataifa nchini Marekani, na Umoja wa Mataifa kwa harakati zake za kumkomboa mtoto wa kike.

Mwaka huu wa 2018 umeanza na hakika wanawake wengi wanaendelea kufanya juhudi mbalimbali katika kujikomboa, tusubiri tuone wale watakaokuwa wanawake wa kuigwa kwa mwaka 2018.

XS
SM
MD
LG