Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:52

Serikali ya Iran yaahidi kupambana na wavunjaji sheria


Waandamanaji nchini Iran wakipinga serikali yao.
Waandamanaji nchini Iran wakipinga serikali yao.

Rais Hassan Rouhani wa Iran ameahidi kuwa vyombo vya usalama vitambana na wanaoleta “vurugu na kuvunja sheria.”

Mamia ya waandamanaji wamekamatwa tangu kuanza kwa maandamano hayo wiki iliyopita yakilaumu hali mbaya ya kiuchumi nchini humo na miradi ya pamoja ya kijeshi baina yake na Syria, Iraq na Yemeni ikiwa ni sehemu ya vita na Saudi Arabia katika kupanua himaya zao katika eneo.

Televisheni ya taifa ya Iran imeripoti kuwa watu kumi wameuwawa usiku uliopita wakati wa maandamano yakupinga serikali ya Iran.

Televisheni ya taifa imesema, “ Baadhi ya waandamanaji waliokuwa na silaha walijaribu kuteka baadhi ya vituo vya polisi na vituo vya jeshi, lakini walikabiliwa na kizuizi imara cha vikosi vya usalama vya nchi hiyo.”

Rouhani ametangaza, “Serikali hiyo haitavumilia wale wanaoharibu mali za taifa, kujihusisha na uvunjaji wa sheria na kusababisha taharuki katika jamii.”

Katika hotuba yake kwa viongozi wa bunge, Rouhani amezilaumu nchi za kigeni, ikiwemo Marekani, Israel na hasa Saudi Arabia, akidai kuwa ndiyo waliochochea machafuko hayo Iran.

“Maendeleo yetu na mafanikio yetu katika ulimwengu wa siasa na dhidi ya Marekani na Utawala wa mabavu wa Kisahyuni hauwezi kuvumiliwa na taifa hilo,” amesema, wakati akiinyoshea kidole Riyadh kwa tamko lake la “waziwazi” kuwa itasababisha matatizo ndani ya jiji la Tehran.

Lakini Rais wa Marekani Donald Trump alipuuzia mbali maelezo ya kiongozi wa Iran, akisema katika ujumbe wa Twitter wa maadhimisho yam waka mpya kuwa “wakati umefika wa mabadiliko” nchini Iran.

“Iran inaporomoka katika kila hatua, pamoja na makubaliano ya ovyo yaliyofikiwa kati yao na Uongozi wa Obama,” Trump amesema, akirejea makubaliano ya kimataifa ya 2015 yaliyokuwa na dhamiri ya kuzuia utengenezaji wa silaha za nyuklia unaofanywa na Tehran, ambapo Tehran kwa kusitisha utengenezaji wa silaha hizo, ingeondolewa vikwazo vya kiuchumi.

“Watu watukufu wa Iran wamekuwa wakikandamizwa kwa miaka mingi. Wananjaa ya chakula na uhuru. Pia wanataka haki za binadamu zitekelezwe na rasilmali za Iran zinaibiwa.”

Mpaka sasa idadi ya vifo ni 12 tangu maandamano hayo yaanze mara ya kwanza Alhamisi iliyopita huko mji wa Mashhad, mji mkuu wa pili Iran, na baadae kuenea maeneo mengine ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG