Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:51

Watu 10 wauwawa katika maandamano Iran


Polisi wakiwazuia wanafunzi kuandamana nchini Iran
Polisi wakiwazuia wanafunzi kuandamana nchini Iran

Television ya taifa ya Iran imesema Jumatatu kwamba watu 10 wameuwawa katika siku moja wakati wa maandamano dhidi ya serikali ambayo yameibuka maeneo mbali mbali ya nchi hiyo tangia wiki iliyopita.

Taarifa hiyo iliyotangazwa haikutoa maelezo zaidi kulingana na vifo hivyo.

Mapema Jumatatu, Shirika la habari la Iran ILNA lilimkariri mbunge wa Iran akisema kuwa watu wawili walipigwa risasi usiku huo katika eneo la kusini magharibi mwa mji wa Izeh, lakini hakuwa anajua nani aliyehusika na kuwapiga watu hao risasi.

Vurugu hizo zinazoendelea zilianza na maandamano madogo Alhamisi iliyopita huko Mashhad, Mji wa pili kwa ukubwa Iran, na ngome ya upinzani dhidi ya rais mwenye msimamo wa kati Hassan Rouhani, kabla ya maandamano kuenea pande nyingine za nchi.

Uongozi wa Trump umesema “umekerwa sana” na kitendo cha Tehran kuzuia Wananchi wa Iran kuwasiliana kwa mitandao ya jamii katika juhudi za kukandamiza maandamano.

Iran imezuia watu wake kutuma ujumbe na kubadilishana picha kupitia mitandao ya Jamii, wakati vyombo vya habari vya taifa vikisema hatua hiyo ilichukuliwa kudumisha amani.

Wairan wamekuwa wakitumia mitandao hii kuwasiliana kuhusu maandamano yanayofanyika mitaani, wimbi kubwa la wananchi likionyesha kutoridhishwa kwao na viongozi wa kidini wa Iran tangu maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyokuwa na utata ya mwaka 2009.

XS
SM
MD
LG