Rais wa Iran, Hassan Rouhani aliwaambia viongozi wa Dunia siku ya Jumatano kwamba hakutakuwa na mashauriano yeyote na Marekani iwapo vikwazo vya kiuchumi vinaendelea kuwepo.
Marekani ilichukua hatua ya vikwazo ikilenga sekta kuu ya mafuta nchini Iran baada ya kujitoa mwaka jana katika mkataba wa mwaka 2015 ambao unadhibiti program ya nyuklia ya Iran.
Utawala wa Trump ulisema kwamba mkataba kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani hayakufanya vya kutosha kuizuia Tehran kuendelea na utengenezaji wa silaha za nyuklia.
Tehran tangu wakati huo ilivuka baadhi ya viwango vilivyowekwa katika mkataba huo ikieleza kwamba mataifa mengine yaliyoshiriki kwenye utiaji saini mkataba huo hayasimamii sehemu ya mkataba huo, hususan katika kuhakikisha Tehran inapata nafuu ya vikwazo.