Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:15

Iran yatungua ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani


RQ-4 Global Hawk
RQ-4 Global Hawk

Iran imetungua ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani Alhamisi katika tukio ambalo maafisa wa Iran wanasema ndege hiyo ilikuwa katika anga ya nchi hiyo, lakini maafisa wa Marekani wamesema ilikuwa katika anga za kimataifa

Kwa maelezo ya Iran, ndege hiyo aina ya RQ-4 Global Hawk ilitunguliwa na majeshi yake ya Revolutionary Guard katika eneo la anga la kaskazini ya jimbo la Hormozgan nchini humo karibu na njia kuu ya meli za kimataifa eneo la Hormuz.

Afisa wa Marekani ameitambua ndege iliyotunguliwa kuwa ni MQ-4C Triton ambayo ilikuwa inaruka katika eneo hilo la Hormuz.

Msemaji wa jeshi la majini la Kikosi cha Central Command cha Marekani Bill Urban ameiambia VOA, "Hakuna ndege ya Marekani iliyokuwa inaruka katika anga la Iran hivi leo."

Alisita kutoa maoni yeyote zaidi juu ya tukio hilo.

Jeshi la Marekani limesema kuwa Iran ilijaribu kutungua ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani wiki iliiyopita, na mvutano huo kati ya nchi hizo mbili umeongezeka kutokana na shambulizi la meli za mafuta katika eneo hilo ambalo Marekani inailaumu Iran kwa tukio hilo, wakati Iran inasema haikufanya shambulizi hilo.

Uhusiano umezidi kuwa mbaya tangu Rais wa Marekani Donald Trump alipojitoa mwaka 2018 kutoka katika mkataba wa kimataifa uliyokuwa unaidhibiti program ya Iran ya nyuklia kwa kupunguziwa vikwazo.

Vikwazo vya Marekani vipya vimeathiri uchumi wa Iran, na Iran imetangaza kuendeleza kuzalisha uranium kwa kuboresha iwe na nguvu hafifu wakati ikitafuta msaada kutoka kwa mataifa ya Ulaya kuzuia hatua hiyo ya vikwazo vya Marekani.

XS
SM
MD
LG