“Tumeanza kuvishambulia vituo vya kikosi cha Quds cha Iran kilichoko katika ardhi ya Syria. Tunaonya majeshi ya Syria juu ya jaribio lolote lile watakalofanya kudhuru majeshi ya Israeli au maeneo yake,” jeshi limetuma ujumbe wa tweet.
Hata hivyo haijatoa maelezo yeyote zaidi.
Lakini Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema wakati wa ziara yake Chad, “Tunayo sera kamili – kuangamiza vituo vya Iran nchini Syria na kumdhuru yeyote anayejaribu kutudhuru.”
Vyanzo vya habari vimeripoti Israel ilifanya mashambulizi hayo ya anga baada ya kuzuia kombora lilorushwa kuvuka milima ya Golan Heights, masaa kadhaa baada ya Syria kusema kuwa makombora kadhaa yalipigwa karibu na uwanja wa ndege wa Damascus.
Israel imesema inataka kujiepusha na kuingilia kati vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria. Imeiomba Russia – mshirika mkuu wa serikali ya Syria – kuyaondosha majeshi ya Iran katika eneo la mpaka kati ya Syria na Israeli.