Hii inakamilisha ziara yake iliyo mchukua katika miji mitatu ya Ulaya akiwa na kusudio la kuwashawishi viongozi wa Ulaya kubadilisha mkataba huo na Iran.
Netanyahu alisimama nchini Ufaransa Jumanne kufanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron na amesisitiza kupinga kwake hatua ya mpango kamili wa pomoja (JCPOA) uliozuia programu ya nyuklia ya Iran na badala yake kuwapunguzia vikwazo.
Kiongozi huyo wa Israeli amesema anachotaka ni kuizuia Iran kupata silaha za nyuklia.
Netanyahu ameeleza: “Sikuitaka Ufaransa kujiondoa katika mkabata wa JCPOA kwa sababu nafikiri JCPOA kimsingi itavunjika kutokana na uzito wa nguvu za uchumi, lakini nafikiri kuna uwezekano wa mambo mawili kutokea: Iran kusimamisha utengenezaji wa nyuklia yenye kutokana na shinikizo hili, au kutakuwa na mazungumzo siku za usoni kwa kuwepo mkataba bora, bora.”
Macron na nchi nyingine za Ulaya wanataka kuendelea na mkataba huu uliopo na Iran, lakini wako tayari kushughulikia mambo mengine na Iran katika mkataba tofauti.
Rais wa Ufaransa amesema : “Mkataba wa JCPOA haujitoshelezi, na nakubali kabisa, lakini bado ni mkataba bora kuliko tulikuwa nayo kabla ya hapo, na vyombo vya ujasusi vya Israeli vimeeleza hilo vizuri sana. Kwa hiyo chukulia kwamba hii inamaana kwamba kunamvutano unaoendelea kati ya nchi hizi na ninamkaribisha kila mtu kuimarisha hali hii na wala kutoongeza mvutano ambao unaweza kupelekea katika mgogoro mkubwa.”
Naye Rais wa Marekani Donald Trump alijitoa kutoka katika mkataba huo, lakini Iran imewataka washiriki wengine waliosaini mkataba huo kuendelea nao.