Katika tamko lililotolewa Alhamisi asubuhi, White House imesema kuwa walinzi wa jeshi la Mapinduzi la Kiislam la Iran (IRGC) “litawajibika kikamilifu kwa matokeo yoyote ya vitendo vyao vya ovyo” na kuonya kuwa jeshi hilo na “wanamgambo wanaopigana kwa niaba yao” wasiendelee kufanya “vitendo vya uchokozi zaidi.”
Israel imesema Alhamisi ndege zake za kivita zilipiga dazeni ya vituo vya kijeshi vya Iran ndani ya Syria usiku wa Jumatano ikiwa ni hatua ya kujibu mashambulizi hayo.
Jeshi la Israeli limesema kuwa shambulizi hilo la anga lililenga vituo vya kijasusi, maghala ya silaha na vituo vya kupanga vita, na kuwa ndege hizo za kivita pia ziliangamiza mifumo ya ulinzi wa anga ya Syria.
Pia Israel imeonya kuwa “haitoruhusu vitisho vya Iran kujikita katika ardhi ya Syria” na wamesema serikali ya Syria itawajibishwa “kwa kila kitu kinachotokea katika ardhi yake.”