Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:03

Netanyahu azuru Ulaya akishawishi Iran idhibitiwe zaidi


Kombora la ballistika linaonekana katika maonyesho ya kijeshi wakati wa maandamano ya siku ya kuwaunga mkono wa Palestina inayojulikana kama Siku ya Al-Quds, Tehran, Iran, Juni 23, 2017.
Kombora la ballistika linaonekana katika maonyesho ya kijeshi wakati wa maandamano ya siku ya kuwaunga mkono wa Palestina inayojulikana kama Siku ya Al-Quds, Tehran, Iran, Juni 23, 2017.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameanza ziara yake Jumatatu katika nchi tatu za Ulaya wakati akitafuta kuungwa mkono juu ya msimamo wake wa kutaka kubadilishwa kwa mkataba wa nyuklia wa kimataifa na Iran.

Netanyahu ataanza ziara yake huko Ujerumani, ambako atafanya mazungumzo na Chansela Angela Merkel kabla ya kuelekea Ufaransa na Uingereza ambako atakutana na viongozi wa nchi hizo.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimekubaliana na mkataba huo wa Iran uliofikiwa mwaka 2015 ukiungwa mkono pia na Russia, China na Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mwezi uliopita kuwa Marekani itajiondoa katika kile alichosema kuwa mkataba huo ni “mbaya, unapendelea upande mmoja,” wakati aliposema anataka vikwazo zaidi juu ya programu ya kombora la ballistika la Iran na kile alichokiita ni “na vitendo vyake vya kuhatarisha hali ya Mashariki ya Kati.”

Wadau wengine waliosaini mkataba huo wameeleza azma yao ya kutaka kuendelea na mkataba huo wa nyuklia, wakisema unafanya kazi. Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wamependekeza kushughulikia kero nyingine zinazoelekezwa kwa Iran kwa kuwepo mkataba wa ziada.

Kama ilivyo kwa Trump, Netanyahu amekuwa akikosoa vikali sana mkataba huo, akisema mkataba huo umeiachia fursa Iran kuwa na uwezo wa haraka kutengeneza silaha ya nyuklia wakati muda wa makubaliano hayo utakapomalizika.

XS
SM
MD
LG