Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:00

Polisi Israeli wataka Netanyahu afunguliwe kesi ya ufisadi


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Jeshi la Polisi nchini Israel Jumapili limetoa pendekezo kuwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na mkewe Sara wafunguliwe mashtaka kwa tuhuma za ulaghai, ufisadi, na kuvunja uaminifu na tayari kumekuwa na shinikizo kuwa lazima ajiuzulu.

Polisi katika uchunguzi wao wamegundua kuna ushahidi wa msingi kufungua kesi dhidi ya waziri mkuu na mkewe juu ya tuhuma hizo.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa Netanyahu na mkewe walishiriki kuipendelea kampuni kubwa ya mawasiliano ili nao waandike habari chanya juu ya waziri mkuu kupitia kampuni tanzu ya habari ,Bezeq, kwenye tovuti yao inayo julikana kama, Walla.

Kesi hiyo inahusu kushukiwa kwa wasiri wake Netanyahu walioshiriki kusukuma kanuni zenye kuipendelea kampuni ya mawasiliano ya Bezeq katika biashara yenye thamani ya mamia ya milioni ya dola za Kimarekani.

Polisi tayari wamependekeza Netanyahu kufunguliwa mashtaka juu ya tuhuma za ufisadi katika kesi nyingine mbili.

Moja inahusu Netanyahu kupokea zawadi za mabilioni ya fedha kutoka kwa marafiki, na ya pili inahusu madai ya kupitisha sheria yenye upendeleo kwa gazeti moja kwa makubaliano liandike habari chanya juu ya Netanyahu.

Waziri Mkuu huyo amekanusha kufanya kosa lolote, akitupilia mbali tuhuma hizo na kuziita ni kutafuta mchawi, na anadai kuwa kampeni hiyo ya kumchafua inaendeshwa na vyombo vya habari.

Mwanasheria mkuu nchini Israel sasa ataamua iwapo afunguwe mashtaka kuhusu madai hayo.

Netanyahu amesema : Pendekezo hili la polisi dhidi yangu na mke wangu halimshangazi mtu yeyote, Mapendezo haya yalishakuwa yameamuliwa na yalivuja hata kabla ya uchunguzi kuanza.”

"Nina imani kuwa katika kesi hii, mamlaka zinazo chunguza suala hili zitafikia uamuzi kuwa hakuna chochote kwa sababu hakuna ushahidi."

Vyombo vya habari nchini Israel vinasema kuwa wachunguzi wamemhoji Netanyahu mara kadhaa.

Netanyahu, 69, anaongoza muungano wenye utata lakini anaamini kuwa madai hayo hayawezi kusukuma kufanyika uchaguzi kabla ya wakati uliopangwa.

Uchaguzi wa bunge umepangwa kufanyika Novemba 19 na Netanyahu yuko katika awamu ya pili ya uongozi wake.

XS
SM
MD
LG