Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:00

Israeli kuwaachilia wafungwa 200 waliohamia kutoka Afrika


Mwanamke wa asili ya Ethiopian akionyesha picha za jamaa yake wakati wa maandamano nje ya bunge la Israeli mjini Jerusalem.
Mwanamke wa asili ya Ethiopian akionyesha picha za jamaa yake wakati wa maandamano nje ya bunge la Israeli mjini Jerusalem.

Wizara ya mambo ya ndani ya Israeli, ilisema Jumapili kwamba serikali itawaachilia huru takriban wahamiaji mia mbili kutoka barani Afrika, huku kukiwa bado hakuna muafaka kuhusu kuhamishwa kwao pamoja na maelfu ya wahamiaji wengine kutoka Eritrea na Sudan ambao waliingia nchini Israeli kinyume cha sheria.

Serikali ya Israeli imekuwa ikijaribu kufikia makubaliano na Uganda, ikiitaka nchi hiyo ya Afrika Mashariki iwapokee wahamaiaji hao, ambao waliingia nchini Israeli kwa kuvuka mpaka wa misri na nchi hiyo kwa miguu katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita.

Shirika la habari la Reuters lilripoti Jumapili kwamba wengi wa wanaume hao mia mbili ambao wako karibu kuachiliwa, wamekuwa wakizuiliwa kwenye jela iliyo jangwani katika kipindi cha miezi michache iliyopita, wakisubiri kuhamishiwa nchini Uganda.

Siku ya Ijumaa, kwa mara ya kwanza, Uganda ilikiri kwamba inafanya mazungumzio na Israeli kuhusu suala hilo, lakini ikasema kuwa itawapokea tu wakimbizi ambao wataondoka Israeli kwa hiari yao na wala siyo kwa kuzlazimishwa.

Waziri wa majanga na maswala ya wakimbizi wa Uganda Musa Ecweru, alinukuliwa akisema kwamba Israel imeomba Uganda kuwapatia hifadhi wahamiaji wapatao mia tano walowasili kati ya mwaka 2006 na 2012.

Akizungumza na waandishi habari, waziri huyo alikanusha habari kwamba kuna mikataba ya siri kati ya Uganda na Israel kuhusiana na suala hilo. Alisema maombi ya watu hao 500 yanayojadiliwa hivi sasa yatakaguliwa kwa kina.

Ripoti ya shirika la kushughulikia wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR, ilisema kwamba waafrika 4,000 waliokuwa wakitafuta hifadhi, wameondoka Israel kwa hiyari na kuelekea Uganda na Rwanda tangu mwaka 2013, ripoti ambayo Uganda na Rwanda zimekanusha.

XS
SM
MD
LG