Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:35

Israel yafurahishwa na ‘mabadiliko chanya’ Marekani


Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu- Waziri wa Ulinzi Jim Mattis
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu- Waziri wa Ulinzi Jim Mattis

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis Jerusalem, amesema kuwa Waisraeli “ wanahisi mabadiliko makubwa” yametokea Marekani.

Kufika kwa Mattis Israeli ni ziara ya kwanza ya kiongozi katika Baraza la Mawaziri la serikali mpya ya Trump.

“Nafikiri hii ni ziara ya kukaribisha mabadiliko chanya, mabadiliko ya kimkakati ya uongozi wa Marekani na sera za Marekani,” amesema Netanyahu.

Mattis alikutana na Netanyahu na Rais wa Isreali Reuven Rivlin baada ya kuongea na Waziri wa Ulinzi wa Israeli Avigdor Leiberman huko Tel Aviv.

Lieberman amempongeza Mattis “kwa hatua za wazi na zenye nguvu dhidi ya Korea Kaskazini, Syria na Iran.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema kuwa Israel na Marekani zinamaadui wanaofanana katika wapiganaji wa Kiislamu, na ameahidi “kufanya kile kitachowezekana” kufikia amani.

Amesema ni pamoja na kulitokomeza kundi la Islamic State na kukabiliana na Iran, ambapo Mattis ameendelea kusema inaitishia Israeli na majirani zake kwa makombora ya ballistiki, kupitia harakati za majini na kwa kutumia washirika wake kama vile Hezbollah, kikundi cha kigaidi ambacho kinamsaidia Rais Bashar al-Assad kuendelea kubakia katika madaraka.

“Nafikiri ni muhimu kujikumbusha kuwa iwapo watu wema hawataungana pamoja, basi watu waovu wanaweza kuleta maangamivu duniani, na tunajukumu kuzuia hilo na kufanya kinachowezekana ilikuhakikisha tunarithisha amani na uhuru kwa vizazi vijavyo,” Mattis amesema.

Kushambuliwa kwa Syria

Viongozi wa Israeli wamelipongeza shambulizi lililofanywa na Marekani likilenga uwanja wa ndege wa Syria mwezi huu, kwa kujibu kitendo cha Assad kutumia silaha za kemikali dhidi ya wananchi.

Syria imehamisha vifaa vyake tangu Marekani iliposhambulia na kuangamiza ndege zake za kivita 20, Mattis amethibitisha hilo katika mkutano na waandishi wa habari huko Tel Aviv mapema Ijumaa.

“Hakuna shaka wamezitawanya ndege zao katika siku hizi za karibuni,” amesema.

Syria na Iraq ndio zitachukua nafasi ya juu katika mazungumzo na viongozi mbalimbali wakati Mattis ataposimama katika ziara yake, Qatar, ambayo inaweka ndege za Marekani za kivita zinazotumika katika kupambana na wapiganaji wa Islamic State.

XS
SM
MD
LG