Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:16

Meli za Japan zahujumiwa Rasi ya Oman


Moja ya meli za mafuta zilizoshambuliwa katika Rais ya Oman, ikionyeshwa wakati mmiliki wake alipokutana na waandishi wa habari Juni 13, 2019. ( Kyodo/via REUTERS ).
Moja ya meli za mafuta zilizoshambuliwa katika Rais ya Oman, ikionyeshwa wakati mmiliki wake alipokutana na waandishi wa habari Juni 13, 2019. ( Kyodo/via REUTERS ).

Jeshi la Majini la Marekani limesema lilikuwa linaendelea kutoa msaada Alhamisi baada ya meli mbili za mafuta kushambuliwa katika Rasi ya Oman.

Manuari ya Marekani US Fifth Fleet yenye kituo chake Bahrain ilipokea taarifa kutoka meli hizo mbili za mafuta kuwa ziko hatarini.

Shirika la habari linaloendeshwa na serikali ya Iran limeripoti kuwa jeshi la majini la Iran liliweza kuwaokoa mabaharia 44 kutoka katika meli hizo na vyombo vyote viwili vilikuwa vinawaka moto.

Rasi ya Oman iko karibu na njia kuu inayopita meli zinazobeba mafuta ghafi, ambayo iko kati ya Rasi ya Uajemi na Rais ya Oman.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Javad Zarif, ambaye alikuwa mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliyetembelea Iran wiki hii, amesema kupitia akaunti yake ya Twitter : Dhana haitaanza kueleza nini kinaweza kuwa kilitokea asubuhi hii.”

Habari zaidi zinasema kuwa meli hizo zina mafungamano na Japan.

Mwezi uliyopita, Umoja wa Falme za Kiarabu uliituhumu Iran kwa kuweka mabomu ili kulipua meli za mafuta nje ya pwani ya UAE. Iran hata hivyo ilikanusha kuhusika na shambulizi hilo.


XS
SM
MD
LG