Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:04

Pompeo atetea ruhsa ya nchi nane kununua mafuta Iran


Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo
Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ametetea hatua ya uongozi wa Trump kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran akijibu hoja ya Warepublikan waconservative wenye msimamo mkali wakidai kuwa alitakiwa aweke vikwazo zaidi ya hivyo ili kuitenga nchi hiyo.

Katika mahojiano na kipindi cha televisheni Jumapili “Fox News Sunday,” Pompeo hajasema ni nchi gani zilizo ruhusiwa na Marekani kukiuka vikwazo hivyo kwa kuendelea kununua mafuta kutoka Iran.

Amesema kuwa zilizo ruhusiwa ni nchi nane ambazo hazijatajwa majina “tunahitaji muda kidogo zaidi kufikia idadi ya sifuri.”

Pompeo amesema kuwa pamoja na kuondolewa vikwazo hivyo kwa kuruhusu nchi hizo kununua mafuta, “ vikwazo hivi dhidi ya Iran tayari vimekuwa na athari kubwa.

Rais Donald Trump aliiondosha Marekani mwaka 2018 kutoka katika makubaliano ya nyuklia ya Iran yalioridhiwa 2015. Vikwazo hivyo vitaanza kutekelezwa Jumatatu.

Pompeo amesema sera ya Trump ya “ kuweka shinikizo la juu kabisa dhidi ya Iran itaendelea kufanya kazi kikamilifu kuanzia kesho.”

XS
SM
MD
LG