Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:38

Zarif aonya utashi wa vita wakati Marekani ikiihusisha Iran na shambulizi la Saudi Arabia


Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ameonya Alhamisi wale wanaofikiria kuishambulia Iran ikiwa ni kulipiza kisasi dhidi ya shambulio la vinu vya mafuta nchini Saudi Arabia, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo kuilaumu moja kwa moja Iran na kusema kile kilichotokea Saudi Arabia ni shambulizi la kivita.

Zarif, akiandika katika akaunti yake ya Twitter, ametaja kuwa kikundi alichokiita “ kikundi B” chenye maafisa wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anaona kuwa kinadhamira ya kuanzisha vita dhidi ya Iran. Amesema wanajaribu “kumdanganya” Rais Donald Trump ili waanzishe vita.

“Kwa maslahi yao, waombe kuwa hawatopata kile wanachokitafuta,” Zarif amesema Alhamisi. “Mpaka hivi sasa wanalipa kwa vita ndogo tu ya Yemen ambayo walikuwa na kiburi cha kusitisha vita hiyo miaka minne iliyopita.”

Pompeo yuko Abu Dhabi kwa ajili ya kuendeleza mazungumzo Alhamisi juu ya kujibu mashambulizi ambayo yameathiri uzalishaji wa mafuta ghafi ya kila siku kwa kipindi kifupi kufikia mapipa milioni 5.7, ambayo ni upungufu wa asilimia 6 ya usambazaji wa mafuta ulimwenguni.

Baada ya kukutana Jumatano na maafisa wa Saudi Arabia, Pompeo alisema : “ Marekani inasimama na Saudi Arabia na wanaounga mkono haki yake ya kujilinda. Mwenendo wa utawala wa Iran wa vitisho hauwezi kuvumiliwa.

Pompeo amekuwa kati ya maafisa wa uongozi wa Trump ambao wamekuwa wakitangaza kuilaumu Iran. Pompeo amewaambia waandishi wanaosafiri naye, “Haya ni mashambulizi yaliyofanywa na Iran,” na kutupilia mbali madai yaliyotolewa na kikundi kinachoungwa mkono na Iran cha Wahouthi waasi wa Yemen kwamba wao walihusika.

Trump alisema Jumatano kuwa Marekani “ina njia nyingi” ikiwemo mashambulizi ya kijeshi ikiwa ni hatua ya kujibu shambulizi la Iran.

“Tuko na nafasi yenye nguvu,” Trump amewaambia waandishi katika eneo ndege ilipoegeshwa uwanja wa ndege wa California wakati akielekea katika harambee ya kisiasa ya kukusanya fedha.

Tamko la Trump limetolewa masaa machache baada ya kusema anaongeza kwa “kiwango kikubwa” vikwazo vya uchumi dhidi ya Iran kufuatia shambulizi la vinu vya mafuta ambalo Washington inasema limetekelezwa na Tehran.

XS
SM
MD
LG