Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:01

Netflix yasitisha onyesho la vichekesho linalo mkosoa Prince wa Saudia


FILE - Saudi Crown Prince Mohammed bin Salman attends the second day of the Future Investment Initiative conference, in Riyadh, Saudi Arabia.
FILE - Saudi Crown Prince Mohammed bin Salman attends the second day of the Future Investment Initiative conference, in Riyadh, Saudi Arabia.

Kampuni inayorusha habari Netflix imeondosha kutoka katika huduma zake nchini Saudi Arabia sehemu ya onyesho la vichekesho ambalo linamkosoa Prince wa Saudia Mohammed bin Salman.

Kipindi hicho kinacho julikana kwa jina la “Patriot Act with Hasan Minhaj” kimeendelea kuonyeshwa katika matangazo yanayo rushwa Marekani tangu Octoba, na kiliondolewa katika matangazo ya kampuni hiyo nchini Saudi Arabia wiki iliyopita.

“Tunaunga mkono kwa nguvu zote uhuru wa kazi za wasanii na tuliondosha oneysho hili katika matangazo yanayorushwa Saudi Arabia baada ya kupokea ombi la kisheria likitutaka tusitishe – na kufuata sheria za nchi hiyo,” Netflix imesema katika tamko lake.

Jarida la Financial Times limeripoti kuwa Tume ya Mawasiliano na Habari ya Saudi Arabia ili fungua malalamiko juu ya kipindi hicho cha vichekesho.

Minhaj ambaye huendesha kipindi hicho katika onyesho hilo la kila siku ambalo ni maarufu kwenye Netflix na amekuwa muandaaji wa hafla ya chakula cha usiku kwa waadishi wa habari wanaoripoti kutoka White House kabla ya kuanzisha kipindi chake mwenyewe mwaka 2018, amekuwa akijadili shutuma kadhaa dhidi ya Saudi Arabia na Prince Mohammed.

Hizi ni pamoja na tuhuma za mauaji ya Octoba ya mwandishi wa gazeti la Washington Post Jamal Khashoggi kwenye ubalozi mdogo wa Saudia, Istanbul, Uturuki.

Saudi Arabia ilitoa maelezo mbalimbali juu ya kifo cha Khashoggi kabla ya kukiri kuwa aliuwawa ndani ya ubalozi huo, lakini wakidai kuwa hilo lilifanywa na wahuni na wala halikuamrishwa na Prince mwenyewe.

XS
SM
MD
LG