Pia amewataka wamtaje mtu aliyetorosha mwili wa mwandishi huyo, baada ya kuuwawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, nchini Uturuki.
Wakati akikutana na wanachama wa chama chake cha AK bungeni, Edorgan amesema kwamba Ankara ina ushahidi kuhusiana na mauaji ya mwandishi Khashoggi, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Edorgan amesema kwamba mwendesha mashtaka mkuu wa Saudi Arabia, atatembelea Istanbul, Jumapili, ili kukutana na maafisa wa Uturuki kama sehemu ya uchunguzi wake.
Saudi Arabia imekiri kwamba mauaji ya Khashoggi yalipangwa, kwa kuzingatia ushahidi ambao umetolewa na Uturuki.
Jambo lisilo julikana ni nani walio muuwa mwandishi huyo. Washukiwa 18 tayari wamekwisha kamatwa nchini Saudi Arabia.