Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:20

Trump asema inavyoelekea Khashoggi hayuko hai


Jamal Khashoggi
Jamal Khashoggi

Rais Donald Trump amesema mwandishi wa habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi "bila shaka inaelekea" kama ameuwawa na hilo ni jambo la "kusikitisha sana."

Trump alijibu kwa kusema inavyo onekana bila shaka amefikwa na maswaiba hayo, akisema inasikitisha. Akizungumza katika eneo la uwanja wa ndege wa jeshi la anga wa Joint Base Andrews kabla ya kupanda ndege ya rais Air Force One

Trump aliahidi kwamba kutakuwa na adhabu kali ikiwa uongozi wa Saudia walihusika na mauwaji yake.

Utawala wa Trump hata hivyo uko tayari kuupatia utawala wa Saudi Arabia muda zaidi kukamilisha uchunguzi wao kutokana na tuhuma zilizo tolewa na Uturuki kwamba maafisa wa ujasusi kutoka utawala wa Kifalme walimuwa Khashoggi ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.

Waziri wa Mambo nje wa Marekani Mike Pompeo baada ya kukutana na viongozi wa Saudia na Uturuki wiki hii alizungumza na Trump jana White House na kumuomba atoe muda zaidi kwa Saudi Arabia ili kumaliza uchunguzi wa kutoweka kwa mwandishi wa habari wa Saudia aliyekuwa akiishi Marekani.

XS
SM
MD
LG