Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:14

Trump azungumzia hatma ya madai ya kuuwawa Khashoggi


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump Jumamosi amesema hatma ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia aliyetoweka Jamal Khashoggi “haitoi picha nzuri kabisa," akisema huenda akawa ameuwawa.

Khashoggi, ambaye makala zake zilikuwa zinamkosoa Prince mwenye madaraka makubwa Mohammad bin Salman, ametoweka tangu alipoingia ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Istanbul Oktoba 2.

“Nafikiri ingekuwa tayari tumefahamu hivi sasa. Hayo yalikuwa matumaini yetu. Matumaini yetu ya awali ni kuwa alikuwa hajauwawa, lakini pengine haitoi sura nzuri kabisa, … kutokana na yale tunayo yasikia,” Trump aliwaambia waandishi wa habari White House.

Trump pia amesema Marekani itakuwa “inajiadhibu yenyewe” iwapo itasitisha mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia, hata kama ikibainika kuwa Khashoggi alikuwa ameuwawa.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS katika kipindi cha 60 Minutes, Trump amesema, “ Tutalifuatilia suala hili kwa kina kujua “kilicho mtokea Khashoggi,” na kutakuwa na adhabu itakayo chukuliwa” iwapo atakuwa ameuwawa.

Trump amesema kuwa “hakuna anayejua uhakika, lakini pengine tutakuja kugundua” iwapo bin Salman aliamrisha kuuwawa kwa Khashoggi. Trump ameongeza kuwa Marekani “itasikitishwa na kughadhibishwa iwapo hilo limetokea.

XS
SM
MD
LG