Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:32

Mwandishi wa Saudia aliye toweka alikuwa 'hatarini' - Mchumba


Wanaharakati wakilaani kupotea kwa mwandishi wa Saudi Arabia nje ya Ubalozi mdogo wa Saudia nchini Uturuki.
Wanaharakati wakilaani kupotea kwa mwandishi wa Saudi Arabia nje ya Ubalozi mdogo wa Saudia nchini Uturuki.

Mchumba wa mwandishi wa habari wa Saudi Arabia ambaye ametoweka baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudia, Istanbul, wiki iliyopita, amesema kuwa mwandishi huyo “alikuwa kwa namna fulani ana wasiwasi wa kuwa hatarini,” lakini hata hivyo hakuogopa kitu chochote kitamtokea katika ofisi hiyo ya kidiplomasia.

Gazeti la Washington Post

Hatice Cengiz ameandika katika gazeti la Washington Post kuwa mchumba wake, Jamal Khashoggi, kwanza alikwenda ubalozini Septemba 28 na kurejea wiki iliyopita baada ya kupewa miadi ya kuchukuwa makaratasi yake ambayo ni kibali cha kufunga ndoa. Tangia wakati huo hakuonekana tena.

Cengiz ameeleza ana imani ya uwezo wa vyombo vya usalama vya Uturuki katika kutafuta kile kilicho msibu Khashoggi, na pia amemtaka Rais wa Marekani Donald Trump “kusaidia katika kadhia” ya mwandishi huyu aliyetoweka.

Pia amesisitiza kuwa viongozi wa Saudi Arabia walazimishwe kuonyesha video za kamera za ulinzi zilizo kuwa zikirikodi eneo hilo wakati mwandishi huyo alipoenda ubalozini.

Tamko la Saudi Arabia

Saudi Arabia imesema kuwa Khashoggi aliondoka ubalozini na kukanusha tuhuma zilizo tolewa na maafisa wa Uturuki ambao wanadai aliuwawa ndani ya ubalozi huo. Hakuna upande wowote uliothibitisha maelezo walio yatoa juu ya kile kilicho tokea.

Khashoggi alikuwa ni mwenye kuikosoa serikali ya Salman, katika Makala zake kadhaa zilizo chapishwa katika gazeti la Washington Post juu ya Prince Mohammed bin Salman, na amekuwa akiishi ugaibuni kwa miaka kadhaa ambako ameamua kuwa mkimbizi bila ya kulazimishwa huko Marekani baada ya Riyadh kuanza kuwakamata wapinzani nchini Saudi Arabia.

Mchapishaji wa gazeti la Washington Post Fred Ryan amelitoa ombi la gazeti hilo la hivi karibuni Jumanne linalotaka taarifa zaidi zitolewe, akisema siyo Saudi Arabia wala Uturuki imetoa maelezo ya kuridhisha.

“Ukimya, ukanushaji na kuchelewesha taarifa havikubaliki. Tunataka kujua ukweli,” Ryan amesema katika tamko rasmi.

Gazeti la Uturuki

Gazeti la upande wa serikali ya Uturuki linaloitwa Sabah limesema Jumatano imelitambua kundi la Wasaudi 15 ambao wanadaiwa kuwa walikuja Istanbul siku ambayo Khashoggi alitoweka, na baadae siku hiyo hiyo waliondoka nchini.

Askari wa Uturuki wamekuwa wakichunguza ndege mbili binafsi ambazo zinaaminiwa kuwa zilikuwa zimebeba kikundi hicho wakati walipo wasili uwanja wa ndege wa Istanbul Octoba 2. Sabah limeripoti kuwa ndege zote mbili zilirejea Riyadh, na moja wapo kusimama kwanza Dubai na nyengine Misri. Ndege hizo zinamilikiwa na kampuni ya Saudia ambayo ina mafungamano na serikali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema Jumanne kuwa vyombo vya usalama vitapekuwa ubalozi mdogo wa Saudia, lakini mpaka sasa hakuna maelezo yoyote wakati gani zoezi hilo litafanyika.

Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amewaambia waandishi wa habari White House kuwa ana mpango wa kuzungumza na utawala wa Saudi Arabia juu ya kutoweka kwa mwandishi huyo, lakini hakuwa na taarifa yoyote juu ya hatma ya Khashoggi.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema maafisa wa Saudia wanalazimika kuthibitisha kuwa Khashoggi aliondoka ubalozini.

“Ni lazima tupate matokeo ya uchunguzi huu haraka iwezekanavyo. Maafisa wa ubalozi hawawezi kujiaminisha kwa kusema kirahisi kuwa, “mwandishi aliondoka ubalozini,” Erdogan amesema Jumatatu alipokuwa ziarani huko Budapest.

Prince Mohammed bin Salman wa Saudia aliyoko madarakani amesema wiki iliyopita kuwa Riyadh “iko tayari kukaribisha serikali ya Uturuki kufanya upekuzi katika jengo letu,” kwa sababu “hatuna kitu cha kuficha” juu ya mwandishi aliyetoweka.

XS
SM
MD
LG