Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:32

Hariri afunguka kuhusu ziara yake Saudia


Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri akiwa na Mrithi wa Ufalme nchini Saudi Arabia Mohammed bin Salman.
Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri akiwa na Mrithi wa Ufalme nchini Saudi Arabia Mohammed bin Salman.

Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri amesema Ijumaa amekuwa Saudi Arabia, ambako alikuwa katika mazungumzo yanayohusu mustakbali wa eneo hilo.

Vyanzo vya habari vimeripoti Hariri aliushitua ulimwengu kwa kutangaza kujiuzulu kwake akiwa nje ya nchi yake.

“Kuwepo kwangu Saudi Arabia ni kwa ajili ya kufanya mashauriano juu ya mustakbali wa Lebanon na mahusiano yake na nchi jirani za Kiarabu,” aliandika katika akaunti yake ya Twitter kabla ya kuanza safari yake kuelekea Ufaransa.

Hariri aliongeza kuwa taarifa nyingine zozote kuhusu uwepo wake Riyadh, kuondoka kwake Lebanon au kuhusu familia yake ni “uzushi”.

Hariri amekuwako nchini Saudi Arabia tangu alipotangaza kujiuzulu mapema mwezi huu, akiibua maswali kuhusu ukweli juu ya kushikiliwa kwake Saudia na kupelekea Rais wa Lebanon Michel Aoun kutangaza kuwa anazuiliwa na utawala huo.

Aoun amesema hatakubali kupokea rasmi kujiuzulu kwa Hariri mpaka atapofika Lebanon.

Waziri wa Mambo ya Nje Adel al- Jubeir Alhamisi alitupilia mbalia madai yasiyo na msingi kuwa Saudi Arabia ilikuwa inamshikilia Hariri na ni juu ya Hariri mwenye kuamua wakati gani anataka kuondoka.

Hariri amekubali mualiko wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenda Ufaransa katika siku zijazo.

XS
SM
MD
LG