Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:41

UN yaitaka Saudia kuruhusu misaada ya kibinadamu Yemen


Wasichana wakifarijiana baada ya nyumba yao kupigwa mabomu karibu na Wizara ya Ulinzi ya Yemen na majeshi ya ushirika yanayoongozwa na Saudi Arabia Sanaa, Yemen, Nov. 11, 2017.
Wasichana wakifarijiana baada ya nyumba yao kupigwa mabomu karibu na Wizara ya Ulinzi ya Yemen na majeshi ya ushirika yanayoongozwa na Saudi Arabia Sanaa, Yemen, Nov. 11, 2017.

Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, kwa mara nyingine tena, yametoa wito kwa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia, kuondoa vikwazo dhidi ya Yemen.

Vikwazo hivyo ambavyo vimesitisha uingizaji wa bidhaa muhimu nchini Yemen, na kuonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini.

Viongozi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Shirika la Afya duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), walisema katika taarifa ya pamoja Ijumaa, kwamba gharama ya vikwazo hivyo inapimwa kwa idadi ya watu waliopoteza maisha yao.

Aidha mashirika hayo yamesema kuwa takriban watu milioni saba wako katika hatari ya kufa njaa nchini Yemen, na idadi hiyo huenda ikaongezeka na kufikia Zaidi ya milioni tatu. Taarifa hiyo imeeleza mzozo huo kama ni mgogoro uliokuwa mbaya zaidi duniani.

Wiki iliyopita, muungano huo udhibitinjia za angani, ardhini na maji, kuingia Yemen, kufuatia shambulizi la kombora, lililotekelezwa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, karibu na mji mkuu wa Riyadh.

XS
SM
MD
LG