Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:30

Saudia yaruhusu misaada ya dharura Yemen


Wanawake walioachwa bila ya makazi wakiwa katika kambi za muda nchini Sanaa,Yemen kutokana na vita.
Wanawake walioachwa bila ya makazi wakiwa katika kambi za muda nchini Sanaa,Yemen kutokana na vita.

Ndege tatu zilizobeba misaada ya dharura na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu zimewasili mjini Sanaa, makao makuu ya Yemen.

Msaada huo ni wa kwanza kuruhusiwa ndani ya nchi katika kipindi cha wiki tatu baada ya ushirika wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia kuiwekea nchi hiyo vikwazo ambapo ilizuia bidhaa muhimu zote kuingia nchini.

Viongozi wa Shirika la Chakula Duniani, Shirika la Afya Duniani na UNICEF walionya kuwa athari za kuzuiwa bidhaa muhimu kuingia nchini humo “ itapelekea kupoteza maisha ya watu wengi.”

Mashirika hayo yalisema kuwa watu milioni 7 wako katika hatari ya kukabiliwa na njaa nchini Yemen na idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Takriban watoto milioni 1 wanahatari ya kukabiliwa na virusi ambavyo huzuia mtoto asiweze kupumua, iwapo maambukizo hayo hayatadhibitiwa, mashirika hayo yameeleza.

Pia wameonya kuwa kunauwezekano kwa kuzuka kipindupindu, ambacho kimepungua tangu kutokea kwa milipuko ya maradhi sugu ambapo kulikuwa na zaidi ya wagonjwa 900,000 katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Ushirika wa unaongozwa na Saudi ulifunga mipaka ya angani, baharini na nchi kavu inayoelekea Yemen kwa kujibu shambulizi la kombora lililotupwa karibu na mji mkuu wa Saudia, Riyadh na waasi wa kikundi cha Houthi kinachosaidiwa na Iran.

Vita vya Yemen vimeuwa zaidi ya watu 10,000 na kuwaacha watu takriban milioni 3 bila makazi. Hata kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza mwaka 2015, Yemen ilikuwa ni nchi ya kiarabu maskini kuliko zote katika dunia.

XS
SM
MD
LG