Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:41

Marekani yasema itasaidia katika upelelezi wa mwandishi wa Saudia


Jamal Khashoggi
Jamal Khashoggi

Marekani imeahidi kusaidia katika upelelezi juu ya kutoweka kwa mwandishi wa habari wa Saudi Arabia katika mazingira ya utatanishi.

Jamal Khashoggi, mkosoaji mkuu wa mwana wa mfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman, alionekana mara ya mwisho, wiki moja iliyopita, akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia Arabia, mjini Istanbul, Uturuki.

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, amesema kwamba Marekani ipo tayari kuwatuma maafisa wa Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (FBI) kusaidia katika upelelezi wa aina yoyote unao hitajika.

Pence hata hivyo hajaeleza iwapo msaada wa upelelezi umeombwa na serikali ya Uturuki au Saudi Arabia.

Maafisa wa Uturuki ambao wameanzisha upelelezi wa kina kuhusu kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari, wanasema kwamba wana Imani aliuwawa ndani ya ubalozi, madai ambao Saudi Arabia inasema hayana msingi wowote.

Saudi Arabia haijatoa video yoyote inayoonyesha Khashoggi akiondoka kwenye ubalozi wake.

XS
SM
MD
LG