Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:21

White House inapingana na CIA kuhusu kifo cha Khashoggi


Jamal Khashoggi
Jamal Khashoggi

Trump alipozungumza na wana habari alisema "bado hawajatoa tathmini yeyote, ni mapema mno. Hiyo ilikuwa ni ripoti ya awali lakini pia inawezekana. Tutaona na tutakuwa na ripoti iliyokamilika Jumanne"

Utawala wa Rais Trump unapingana na ripoti ya maafisa wa Marekani wakikariri idara ya ujasusi ya Marekani-CIA kwamba mwana mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman aliagiza mauaji ya mwandishi wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi.

Rais Donald Trump wa Marekani aliarifiwa Jumamosi kwa njia ya simu na mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya serikali kuu ya Marekani-CIA, Gina Haspel na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo wakati rais akiwa ndani ya ndege Air Force One akielekea jimbo la California kushuhudia uharibifu uliosababishwa na moto mbaya katika historia ya jimbo hilo. Baadae Trump alizungumza na waandishi wa habari kuhusu habari iliyochapishwa Ijumaa na gazeti la The Washington Post la Marekani.

Rais Trump akiongea na wanahabari
Rais Trump akiongea na wanahabari

Trump alisema “bado hawajatoa tathmini yeyote, ni mapema mno. Hiyo ilikuwa ni ripoti ya awali lakini pia inawezekana. Tutaona na tutakuwa na ripoti iliyokamilika Jumanne.” Trump alisema wakati huo huo hatua zinachukuliwa dhidi ya watu wanaojulikana kwa hakika walihusika katika tukio hilo.

Tathmini ya CIA iliyoripotiwa kwanza na gazeti la The Washington Post siku ya Ijumaa inapingana na Saudi Arabia ambapo mwendesha mashtaka wa cheo cha juu siku moja kabla alisema mwana mfalme hakuhusika katika mauaji ya Jamal Khashoggi. Maafisa wa Marekani wanasema CIA ilihitimisha kwamba maafisa 15 wa Saudi Arabia katika serikali ya Saudi Arabia walikwenda Istanbul na walimuuwa Kashoggi ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Uturuki.

XS
SM
MD
LG