Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:25

Mauaji ya Khashoggi yazungumziwa Bahrain


Jamal Khashoggi
Jamal Khashoggi

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Jim Mattis, alisema Jumamosi, “mauaji ya Jamal Khashoggi katika jengo la kidiplomasia lazima yatupe wasi wasi sisi sote”. Kushindwa kwa taifa lolote kuambatana na kanuni za kimataifa na utawala wa sheria unadumaza uthabiti wa kieneo katika wakati ambao unahitajika zaidi, Mattis alisema katika maneno yaliyoandaliwa kwenye mkutano wa usalama wa kila mwaka wa Manama Dialogue huko Bahrain.

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Jim Mattis
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Jim Mattis

Mattis alisema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo tayari amesitisha baadhi ya viza za raia wa Saudi Arabia na atachukua hatua ya ziada dhidi ya watu waliohusika.

Wakati huo huo ripoti za habari za Marekani zinasema Salah bin Jamal Khashoggi, mtoto wa kiume wa mwandishi wa habari Jamal Kashoggi aliyeuwawa katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Instabul amewasili nchini Marekani. Kijana huyo raia wa marekani mwenye asili ya Saudi Arabia alizuiliwa na serikali ya Saudi Arabia kuondoka nchini humo mwanzoni mwa wiki hii.

XS
SM
MD
LG