Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:45

Mauaji ya Khashoggi : Ujerumani kutoa katazo dhidi ya Wasaudi 18


Heiko Maas Germany
Heiko Maas Germany

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema Jumatatu kuwa Berlin itapiga marufuku raia 18 wa Saudi Arabia kuingia eneo huru la mipaka ya Ulaya kwa visa ya Schengen kwa sababu ya madai ya kuhusika kwao na kuuwawa kwa mwandishi wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi.

Heiko Maas amesema kuwa ameshauriana na Ufaransa na Uingereza kabla ya kutangaza katazo hilo.

“Kuna maswali zaidi kuliko majibu katika kesi hii, kutokana na uhalifu wenyewe na yule aliyekuwa ameupanga,” Mass amesema pembeni ya mkutano wa Umoja wa Ulaya huko Brussels.

Rais Donald Trump amesema amepewa muhtasari kamili juu ya sauti iliyokuwa imerikodiwa ya mauaji ya mpinzani huyo ambaye ni mwandishi wa habari yaliyotokea katika ubalozi mdogo huko Istanbul mwezi Octoba, lakini hana nia ya kusikiliza sauti hiyo iliyorikodiwa kwa sababu ya ukatili wa kile kilichotokea kama kinavyo sikika.

“Ni sauti ya mateso katika kile kilicho rikodiwa. Ni rekodi yenye kuhuzunisha,” Trump ameiambia Fox News Jumapili katika mahojiano yaliyofanyika na kurikodiwa Ijumaa

XS
SM
MD
LG