Ofisa wa jeshi linalounga mkono serikali ya Yemen alieleza Jumapili kuwa vikosi vinalenga kuwaondoa waasi katika mji ambao wanadhibiti bandari mahala ambako takribani vyakula vyote, dawa na vifaa vingine kwa ajili ya raia vinapelekwa huko.
Wafanyakazi wa msaada wa kibinadamu wana wasi wasi matatizo ya muingiliano wa usambazaji wa mahitaji ya binadamu yatapelekea njaa kali katika nchi ambayo tayari ipo kwenye mwangaza wa njaa.
Saudi Arabia inawashutumu wa-Houthi kwa kutumia bandari hiyo kupitisha vifaa vya kivita vinavyoshushwa na Iran, madai ambayo Iran inakanusha.
Ripoti zinasema raia wasiopungua saba wameuwawa katika mapigano ya mtaani.