Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 06:09

Balozi wa Marekani : Suluhisho la kisiasa ndio ufumbuzi pekee Yemen


Mpiganaji wa kikundi cha Wahouthi akilinda juu ya paa la jengo Sanaa, Yemen, Octoba 5, 2018.
Mpiganaji wa kikundi cha Wahouthi akilinda juu ya paa la jengo Sanaa, Yemen, Octoba 5, 2018.

Vita vinavyo endelea Yemen haviwezi kusuluhishwa kwa mtutu wa bunduki, na kuwa juhudi zinatakiwa zifanyike na pande zote hasimu katika mgogoro huu kutafuta suluhu ya kisiasa, balozi wa Marekani nchini Yemen amekiambia kituo cha TV cha Alhurra kinacho dhaminiwa na Marekani wiki iliyopita.

“Nina amini kuwa kuna fursa siku za usoni inayotokana na mshikamano imara wa kimataifa kuendelea kushinikiza suluhishi la kisiasa,” Balozi wa Marekani Yemen Methew Tueller amesema. Ameongeza kuwa Marekani inataendelea na nia yake ya kutafuta suluhisho la kisiasa katika mgogoro huo katika nchi hiyo iliyo sambaratishwa na vita.

Suluhisho la Kisiasa

“Naamini hatimaye wananchi wa Yemeni wenyewe wanatambua kuwa lazima kuwe na suluhisho la kisiasa,” Tueller amesema.

Ahmed Awad Bin Mubarak, Balozi wa Yemen nchini Marekani, ameiambia VOA kuwa wakati serikali ya nchi yake inaendelea kuunga mkono juhudi za Marekani na Umoja wa Mataifa kutafuta suluhu ya kisiasa katika vita hivyo, shinikizo la kijeshi linahitajika.

“Tuna amini, mpaka hivi sasa, kwamba suluhisho pekee katika mgogoro wa Yemen ni ufumbuzi wa kisiasa. Tuna amini kutokana na uzoefu wetu wa kukabiliana na kundi la Houthi hawatakubali kuja katika meza ya mazungumzo mpaka shinikizo la kijeshi litakapo fika kiwango fulani,” Bin Mubarak amesema.

Mkutano wa Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa umekuwa ukijaribu kusimamia mazungumzo kati ya pande hasimu Yemen ikiwa ni sehemu ya juhudi ya kutafuta suluhu katika mgogoro huo.

Mwezi uliopita, UN iliitisha mkutano wa siku tatu Geneva kuzungumzia jinsi ya kumaliza mgogoro huo, lakini kikundi cha Houthi hawakushiriki.

“Hatukufanikiwa kuuleta ujumbe wa kikundi cha Ansarullah, kuwaleta wawikilishi wao hapa kutoka Sanaa,” Mjumbe maalum wa UN huko Yemen Martin Griffiths amesema, akieleza kusikitishwa kwake kwa hatua ya kikundi cha Houthi kususia mkutano huo.

Lakini Griffiths ameonekana akiwa na matumaini na kusema timu yake itaendelea kuwasiliana na pande zote.

“Tuliendelea na mazungumzo, majadiliano na mipangilio kwa siku zote tatu na kutumia fursa na hatua mbadala kuwaleta wawakilishi wa Houthi hapa,” amesema.

Vipi Iran inahusika Yemen

Wakati huohuo, Balozi Tueller amesema Iran imehusika katika kuzuia wawakilishi wa kikundi cha Houthi kuhudhuria mkutano wa Geneva.

“Ninaona katika mazungumzo mara nyingi, mikakati na mbinu za kikundi cha Wahouthi wamekuwa wakitumia mfululizo njia mbali mbali za mazungumzo yanayo fanyika kimataifa, wanafuata mbinu ambazo tumezizoea kutokana na uzoefu wetu wa kufanya mazungumzo na Iran, kwani siku zote wamekuwa wakifuata utaratibu ambao unafanya mazungumzo kuwa ni magumu,” Tueller amesema.

Lakini amesema Kikundi cha Wahouthi hawako chini ya Iran kikamilifu.

“Inabidi tufanye kazi na wale wa upande wa kitengo cha siasa ya kikundi cha Wahouthi, ambao hawataki kuona Iran au nchi yoyote nyingine ikiingilia kati masuala ya ndani ya Yemen,” Tueller ameongeza.

XS
SM
MD
LG