Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:38

Jeshi la Marekani lakamata silaha Ghuba ya Aden


Begi la silaha aina ya AK-47 limekamatwa kutoka katika Ghuba ya Aden, Agosti 28, 2018.
Begi la silaha aina ya AK-47 limekamatwa kutoka katika Ghuba ya Aden, Agosti 28, 2018.

Jeshi la majini la Marekani limekamata silaha zilizokuwa zinaingizwa kinyume cha sheria katika Ghuba ya Aden, wakati huu ambao vita inaendelea nchini Yemen.

Begi lenye silaha aina ya AK-47 zilikamatwa zikiwa katika boti ya kienyeji iliyokuwa inazisafirisha na zimehifadhiwa katika manuari ya kivita inayo tungua makombora iitwayo USS Jason Dunham iliyo kuwa katika Ghuba ya Aden, Agosti 28, 2018.

“Meli hiyo ya kivita iliyoko pamoja na meli za Marekani za 5th Fleet, imekamata mzigo wa silaha uliokuwa unasafirishwa kinyume cha sheria ukiwa katika chombo ambacho hakimilikiwi na nchi yoyote katika eneo la bahari la kimataifa la Ghuba ya Aden,” Jeshi la majini limesema katika tamko lake. Operesheni hiyo ya kukamata silaha hizo ilifanyika Jumanne.

Tamko hilo la jeshi limesema Manuari ya Dunham iliiona boti hilo ambalo ni usafiri wa kienyeji majini ambao ni aghlabu kutumika katika eneo la Ghuba ya Uajemi, ikihamisha “mizigo iliyokuwa imefungwa” katika chombo kingine kilicho kuwa kinaelea majini.

Chombo hicho kilifahamika kuwa hakina mmiliki kufuatia uhakiki wa bendera iliyokuwa katika chombo hicho uliofanyika kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Jeshi la majini limesema.

Timu ya uchunguzi na ukamataji ya meli ya Dunham ilikuta zaidi ya silaha 1,000 aina ya AK-47 zilizokuwa zimefichwa ndani ya chombo hicho.

Jeshi hilo limesema halijaweza kujua silaha hizo zilitokea wapi, ambazo hivi sasa wanazishikilia.

Chombo hiki chenye injini zilikuwa hazifanyi kazi, kwa mujibu wa jeshi hilo la Majini. “Wanamaji wenye wasiwasi” waliokutwa katika chombo hicho walihamishwa katika manuari ya Dunham na baadae kuhamishwa kwa Walinzi wa Pwani ya Yemen.

XS
SM
MD
LG