Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:05

Askari wa Marekani auwawa Yemen


Jimbo la al-Bayda, Yemen
Jimbo la al-Bayda, Yemen

Jeshi la Marekani limesema askari wake mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi lake lililokuwa limeelekezwa kwa kikundi cha al-Qaida huko Yemen.

"Tumesikitishwa sana na kifo cha askari wetu katika kikosi maalumu cha 'Elite'," amesema kamanda wa Kikosi cha Central Command cha Marekani," Jenerali Joseph Votel.

"Kujitolea huku ni kwa hali ya juu katika vita yetu dhidi ya magaidi ambao wanahatarisha maisha ya watu wasio na hatia ulimwenguni."

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Central Command ya Marekani imesema wapiganaji 14 wa Yemen wenye mafungamano na kundi la al-Qaida waliuwawa katika mashambulizi haya.

Ndege ya kivita ya jeshi la Marekani ilioshiriki katika shambulizi hilo ilishindwa kuendelea na zoezi hilo kwa sababu ya kushindwa kutua na kusababisha matatizo zaidi kwa askari wake, taarifa hiyo imesema ndege hiyo iliangamizwa.

Viongozi wa makabila na vyanzo vya habari vya Yemen vimedai kuwa viongozi wa ngazi ya juu wa al-Qaida walikuwa kati ya wale waliouwawa.

Mashambulizi hayo yalifanyika katika jimbo la Bayda.

.

XS
SM
MD
LG