Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:58

Trump amsifia Prince Salman kwa kuleta mageuzi Saudi Arabia


Rais Trump akiwa na Prince Salman
Rais Trump akiwa na Prince Salman

Rais wa Marekani Donald Trump amempongeza Prince wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman walipokutana katika kikao cha pembeni cha mkutano wa Kundi la Mataifa 20 nchini Japan, akieleza kuwa “ni rafiki yake” ambaye amefanya mambo makubwa.”

Trump amesema Jumamosi kuwa anaridhika na kitendo cha Saudi Arabia kununua vifaa vya kivita vinavyo tengenezwa na Marekani na kusema kuwa Prince amejitahidi kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii katika nchi yake.

Rais wa Marekani alisita kujibu swali kutoka kwa waandishi wa habari iwapo ataibua kero ya mauaji ya mwandishi wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi yaliyotokea mwaka 2018. Prince huyo wa Saudi Arabia ameendelea kukabiliwa na uchunguzi wa kimataifa tangu kuuawa kwa Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Ufalme wa Saudi Arabia mjini Instanbul mwaka 2018.

Kufuatia mazungumzo ya pamoja kati ya viongozi hao wawili Jumamosi, White House imesema mkutano wa viongozi hao ulikuwa na tija, pia walizungumzia tishio linaloongezeka la Iran, ulazima wa kuhakikisha utulivu katika soko la mafuta la kimataifa na umuhimu wa masuala ya haki za binadamu.

Trump pia amepangiwa baadae Jumamosikukutana na Rais wa China Xi Jinping ili kujaribu kuanzisha mazungumzo ya kibiashara tena kati ya nchi hizo yaliyovunjika mwezi uliopita.

Trump alipoulizwa na VOA wakati alipofanya mkutano na Rais wa Brazil Jair Bolsonaro iwapo anatarajia Xi kuja na pendekezo la makubaliano ya kibiashara watakapokutana Jumamosi, alijibu: “Tutaona nini kitatokea kesho. Itakuwa ni siku yenye hamasa, na hakika, kwa watu wengi, na dunia nzima… nimatumaini yangu matokeo ya mkutano yatakuwa na manufaa kwa nchi zote mbili na yataweza kutekelezeka.”

XS
SM
MD
LG