Kura zilikuwa 248 kwa 177 na ni mara ya kwanza kwa baraza hilo kutumia sheria ya War Powers Act.
Uamuzi huo sasa utapelekwa Baraza la Seneti ambalo lilipitisha hatua kama hiyo mwishoni mwa mwaka 2018, na kuwepo uwezekano wa kuzuka mvutano na White House.
Marekani imekuwa ikitoa msaada wa kipelelezi na vifaa kwa ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia unaopigana na waasi wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen.
Vita hiyo imeuwa maelfu ya raia tangu mwaka 2014 na tayari imesababisha janga kubwa la kibinadamu katika moja ya mataifa maskini sana duniani na kufanya hali kuwa mbaya zaidi nchini humo.
Mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Saudi Arabia yanayowalenga waasi yameharibu maeneo ya shule na mahospitali.