Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:27

Yemen: Katibu Mkuu wa UN akutana na wawakilishi wa pande hasimu


Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akikutana na wawakilishi wa pande hasimu katika mgogoro wa Yemen, kwenye mkutano huko Stockholm, Sweden.
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akikutana na wawakilishi wa pande hasimu katika mgogoro wa Yemen, kwenye mkutano huko Stockholm, Sweden.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akutana Alhamisi na wawakilishi kutoka pande hasimu nchini Yemen kabla ya kuhutubia kufungwa kwa duru ya mwisho ya kikao cha mazungumzo ya amani ambapo wasuluhishi wanamatumaini utaleta muendelezo wa mambo muhimu kadhaa.

Guterres amewasili jioni Jumatano huko Sweden ili kuweza kushiriki katika sehemu ya siku ya mwisho wa mazungumzo hayo na kuwapa moyo pande zote kuendeleza yale walioweza kuafikiana mpaka sasa.

Serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wamekubaliana kubadilishana kundi kubwa la mateka wa kivita. Repoti zinasema kuwa wamekaribia kufikia makubaliano kufungua uwanja wa ndege wa Sanaa, na kuanza kuuza gesi na mafuta ili kuwezesha nchi hiyo iliyokwama kiuchumi kuanza kuingiza kipato chake.

Lakini hali hivi sasa katika eneo la bandari ya Hodeida linaloshikiliwa na waasi bado ndio mzizi wa mgogoro huo.

Pande zote mbili zimetupilia mbali pendekezo la kuwaondoa wapiganaji na silaha kutoka katika mji huo na kuusalimisha mji huo chini ya uongozi wa muda wa Umoja wa Mataifa.

Takriban chakula chote na msaada wa kibinadamu unaoletwa unapitia katika bandari hiyo na kuzuiliwa kuingia misaada hiyo unatishia kuifanya hali iwe mbaya zaidi kile Umoja wa Mataifa ilichosema ni hali mbaya kuliko zote ya mgogoro wa kibinadamu.

Ushirika wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia unaosaidia majeshi ya serikali ya Yemen unasema waasi hao wanapata silaha kutoka Iran kupitia bandari hiyo, tuhuma ambayo Iran inakanusha.

Saudi Arabia ilianza kuingilia kati mgogoro wa Yemen kijeshi mwaka 2015 na imeshutumiwa na vikundi vya haki za binadamu kwa mashambulizi yake ya anga kuuwa raia. Vikundi vya haki za bindamu vinawalaumu Wahouthi kwa kukiuka haki hizo pia.

Baraza la Seneti la Marekani imepanga kupiga kura juu ya hatua ya kusitisha misaada ya Marekani kwa jeshi la Saudi Arabia kutokana na kujihusisha kijeshi katika mgogoro wa Yemen.

Pamoja na kuwa wanapinga programu za hizo za kijeshi, wabunge wengi wamekerwa na mauaji ya mwandishi mpinzani wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi, unaodaiwa uliamrishwa na Prince wa Saudia aliyeko madarakani Mohammed bin Salman, na Rais Donald Trump asiykuwa tayari kuukosoa utawala wa Saudi Arabia.

Trump hayuko tayari kumkasirisha mshirika wake mkuu kama Saudi Arabia. Lakini ameiambia Reuters Jumanne, “Nachukia kuona kile kinachoendelea huko Yemen. Lakini inahitaji pande mbili kukamilisha kitu. Ninataka kuona Iran ikijitoa katika mgogoro wa Yemen.

Pande zote mbili katika mazungumzo ya amani hayo zinasema zinapanga kukutana tena mapema mwaka 2019.

Mapigano kati ya Wahouthi na majeshi ya Yemen yalianza mwaka 2014, wakati waasi hao walipouteka mji mkuu wa Sanaa. Zaidi ya watu 10,000 waliuwawa.

XS
SM
MD
LG