Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:13

Saudia yatoa tamko baada ya kushambulia upya Hodeida


Wanajeshi wa serikali ya Yemen wakifanya doria sehemu ambayo wananchi wanaandamana dhidi ya kudorora kwa uchumi wa Yemen na kushuka kwa thamani ya sarafu yake.
Wanajeshi wa serikali ya Yemen wakifanya doria sehemu ambayo wananchi wanaandamana dhidi ya kudorora kwa uchumi wa Yemen na kushuka kwa thamani ya sarafu yake.

Viongozi wa Saudi Arabia na washirika wake wanasema kwamba wanania ya kupunguza uhasama nchini Yemen, siku chache tu baada ya kuanzisha mashambulizi mapya katika mji muhimu wa bandari ya Hodeida, unaotumiwa kuwasilisha msaada wa dharura.

Afisa mmoja wa ushirika huo amesema Jumatatu kwamba wanaunga mkono kwa dhati utaratibu wa kisiasa unaopendekezwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa (UN).

Siku ya Alhamisi iliyopita mungano huo unaongozwa na Saudi Arabia ulianzisha mashambulizi ya anga na ya nchi kavu katika lengo la kuuteka mji wa Hodeida kwenye bahari ya sham unaodhibitiwa na wapiganaji wa Kihouthi.

Mashambulizi yalikuwa yamesitishwa kabla ya kuanza mazungumzo ya amani mjini Geneva ambayo yalivunjika mwezi Septemba 2018.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths anasema hivi sasa ana matumaini ya kupanga mazunguimzo kati ya serikali na wahouthi mwezi huu.

Mapigano ya mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 60 na dazeni kadhaa kujeruhiwa mjini Hodeida.

XS
SM
MD
LG