Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:09

Wasichana wa Saudia inawezekana walijiuwa - Polisi


Wasichana wa Saudia waliopatikana wamekufa ufukweni mwa mto Hudson ulioko jijini New York, Jumanne Octoba 30, 2018. (Picha ya NYPD kupitia shirika la habari AP)
Wasichana wa Saudia waliopatikana wamekufa ufukweni mwa mto Hudson ulioko jijini New York, Jumanne Octoba 30, 2018. (Picha ya NYPD kupitia shirika la habari AP)

Polisi jijini New York wanasema ndugu wa kike wawili wa Saudia ambao miili yao ilikuwa imeletwa na maji ufukweni katika Mto wa Hudson ulioko Mji wa Manhattan kuna uwezekano kwamba walijiuwa.

Mkuu wa idara ya upelelezi ya mji wa New York, Dermot Shea amesema Tala Farea, 16, na Rotana Farea, 23, walisema wanahiari kujiuwa kuliko kurejea Saudi Arabia.

Shea anasema inawezekana wasichana hao “walijitupa ndani ya maji wakiwa hai.”

Miili yao imekutikana imefungwa pamoja, upande wa kiuno na visigino, polisi wamesema.

Kwa mujibu wa ushahidi wa picha ya video, waliotoa ushahidi na manunuzi ya chakula waliofanya kwa kutumia kadi ya benki, hoteli na usafiri, polisi wameweza kujua kuna uwezekano hakukuwa na kitendo cha uhalifu kilicho sababisha vifo vyao.

Wasichana hao ambao walikuwa wameishi nchini Marekani kwa miaka mitatu, inawezekana walikuwa wamedhalilishwa kimwili na huenda waliomba hifadhi ya ukimbizi.

Familia yao inayoishi huko Jimbo la Virginia ilikuwa imekutana nao mwaka 2017.

XS
SM
MD
LG