Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:01

DNA, alama za vidole : FBI yavitumia kumkamata mtuhumiwa Sayoc


Cesar Altieri Sayoc (mwenye shati jeusi), baada ya kakamatwa na maafisa wa FBI
Cesar Altieri Sayoc (mwenye shati jeusi), baada ya kakamatwa na maafisa wa FBI

Masaa kadhaa kabla ya kukamatwa, wakati vyombo vya usalama vya serikali kuu (FBI) vikikaribia kumkamata, na kukusanya ushahidi, mshukiwa Cesar Sayoc alikuwa yuko katika shughuli zake za muziki kama DJ alipokuwa amepata kazi katika moja ya nyumba za starehe akitumbuiza nyimbo maarufu 40.

Umahiri wa wachunguzi

Wakati akiendelea kutumbuiza wateja katika chumba chenye taa yenye mwanga mdogo inayoangalia jukwaa katika klabu ya watu wenye kuheshimika, ambako mapambo ya sikukuu ya Halloween yakining’inia kwa kusubiria sherehe hizo za mavazi, asingeweza kujua kwamba wachunguzi jioni ile walikuwa wanaandaa kesi dhidi yake kwa kutumia makosa aliyoyafanya yeye mwenyewe.

Hana habari uchunguzi unaendelea

Kadhalika bila shaka alikuwa hana hisia yoyote kwamba wataalamu katika maabara walikuwa wamelinganisha kwa kutumia kipimo chake cha DNA na vile vitu vilivyo patikana katika vifurushi venye vilipuzi ambavyo anatuhumiwa kuvituma kwa Wademokrat maarufu kutokana na sampuli zilizo kuwa zimekusanywa na vyombo vya usalama katika jimbo la Florida.

Na pengine alama za vidole zilizofanana na zile za kifurushi cha peke yake ambacho vyombo vya usalama wanasema alikuwa amekituma.

Na pengine alikuwa hana habari kuwa wachunguzi wakipitia akaunti zake za mitandao ya jamii walikuwa wamepata makosa yanayofanana ya maandishi yaliyo kuwa katika ujumbe alioutuma katika mitandao – “Hilary” Clinton, Debbie Wasserman “Shultz” – makossa yale yale yaliokuwa katika vifurushi ambavyo amefunguliwa mashtaka kwa kuvituma.

Viashiria vya uhalifu vinavyo jitosheleza

Mwisho wa yote, waendesha mashtaka waliomfungulia mashtaka Sayoc kwa uhalifu wa makosa matano chini ya sheria ya serikali kuu Ijumaa wanasema mkereketwa anaye muunga mkono Rais Donald Trump bila ya kutambua aliacha nyuma yake viashiria vya kutosha, vilivyo wawezesha kufuatilia kwa makini kwa kufanya uchunguzi kutoka pwani hadi pwani kuchimbua vifurushi vilivyokuwa na vilipuzi vilivyotumwa kwa njia ya posta ambavyo vilisababisha hofu ya kuwepo uvunjifu wa amani katika kipindi cha uchaguzi.

Vifurushi vilidhibitiwa

Vifurushi hivyo vilivyo kuwa vimefungwa madhubuti, vilikuwa vimetumwa kwa Wademokrat kama vile Barack Obama na Hillary Clinton na viliweza kuanza kudhibitiwa wakati vikiwa Delaware mpaka huko California, vilikuwa na ushahidi muhimu wa uhalifu ambao wachunguzi wanasema vilitosheleza kuwa vielelezo vya kumkamataSayoc siku nne baada ya uchunguzi kuanza.

XS
SM
MD
LG