Katika masaa kadhaa, Kituo cha Time Warner huko New York, ambako studio za mtandao wa habari wa CNN ziliko, wafanyakazi waliondolewa kutoka katika jengo hilo Jumatano asubuhi baada kifurushi kinachotiliwa mashaka kukutikana katika chumba ambacho barua zinahifadhiwa.
Kitu hicho kilicho kuwa katika bahasha kiliondoshwa kutoka katika eneo hilo kwa salama katika gari maalum na kikosi cha kutegua mabomu cha idara ya polisi ya mji huo.
CNN imeripoti kuwa kifurushi hicho kilikuwa kimetumwa kwa jina la Mkuu wa Idara ya Ujasusi (CIA) wa zamani John Brennan, mkosoaji wa Trump mwenye hisia za juu ambaye ni mchangiaji wa Shirika la televisheni la MSNBC, ambao ni wapinzani wa mashirika ya habari.
Maafisa wa polisi wa New York wamesema inavyo onekana ni bomu lenye uwezo wa kulipuka na kifurushi kilichokuja nalo kilikuwa na unga mweupe. Meya wa New York Bill de Blassio amesema “kile tunachokiona hapa leo ni kitendo cha kututishia” na kusisitiza kuwa hakuna vitisho vingine vilivyo thibitishwa katika jiji la New York.
Gavana wa New York Andrew Cuomo amewaambia waandishi wa habari kuwa bomu pia lilikuwa limetumwa katika ofisi yake.